Afisa Mtendaji Mkuu wa Simba, Barbara Gonzalez ametangaza kujiuzulu nafasi yake ndani ya klabu hiyo kuanzia mwezi Januari mwakani.
Barbara amehudumu katika nafasi hiyo tangu Septemba 2020 akichukua nafasi ya Senzo Mazingiza aliyejiuzulu nafasi hiyo hiyo.
Taarifa iliyotolewa na Barbara inasema "Leo nimeandika barua ya kujiuzulu wadhifa wangu kama Afisa Mtendaji Mkuu wa Simba kuanzia Januari mwakani," "Nimetoa notisi ya mwezi mmoja ili nishiriki kuhakikisha kipindi kizuri cha mpito (transition) na makabidhiano (handover) na menejimenti mpya,"