KLABU ya Chelsea wanatazamia kukusanya Pauni 500 milioni kutoka kwa taasisi za fedha za Marekani kwa mujibu wa ripoti.
Hiyo ni kwa sababu wapigaji pesa wakubwa wa Stamford Bridge wanatafuta mkopo, kitu ambacho hata klabu zingine za Ligi Kuu England zimefanya katika miaka ya hivi karibuni.
Hatua hiyo inakuja baada ya matumizi makubwa kufanyika katika usajili wa wachezaji chini ya mmiliki mpya Todd Boehly.