MABOSI ya Yanga wamerudi tena kwa mshambuliaji wa kimataifa wa Kitanzania, Simon Msuva wakitaka kufanya mpango wa kumsajili haraka kupitia dirisha dogo baada ya kuachana na klabu ya JS Kabylie ya Algeria.
Mabosi wa Yanga kwa sasa wanapambana kuhakikisha wanamleta straika huyo kutoka Asec Mimosas ya Ivory Coast, Sankara Karamoko kabla ya kuuaga mwaka 2023 kwa lengo la kuimarisha eneo la ushambuliaji ambalo limekosa mtu wa mwisho wa kutupia nyavuni, japo timu imekuwa ikifunga mabao mengi kwenye Ligi Kuu.
Yanga imekuwa ikihusishwa na nyota huyo wa zamani wa Marumo Gallants tangu mwishoni mwa msimu uliopita kabla ya kuibukia Kaizer Chiefs ikielezwa alitangulizwa na Kocha Nasreddine Nabi aliyekuwa mbioni kujiunga na timu hiyo baada ya kutimka Jangwani.
Shekhan amesajiliwa na Yanga kutoka JKU na kutambulishwa juzi kwenye mchezo wa Ligi Kuu wakati timu hiyo ikiinyoosha Mtibwa Sugar kwa mabao 4-1, huku akitajwa kama ndiye mrithi wa Fei kwenye kikosi cha Miguel Gamondi akipewa mkataba wa miaka mitatu.