HII inaweza ikawa taarifa njema kwa mashabiki wa Manchester United, baada ya kusubiri kwa muda mrefu mchakato wa uuzwaji wa klabu yao hiyo.
Rasmi, sasa taarifa zinasema mwekezaji mpya wa klabu hiyo, bilionea Sir Jim Ratcliffe amethibitishwa kuchukua umiliki wa asilimia 25 za hisa za klabu hiyo, kwa Pauni 1.25 bilioni na dili hilo litaifanya kampuni ya INEOS kuhusika na mambo ya uendeshaji wa klabu ikiwamo kuwa na kauli kwenye masuala ya biashara yanayoongozwa na Familia ya Glazers.