YANGA imeondoa gundu la kushindwa kutinga makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika kwa miaka 25 iliyopita baada ya kutinga kibabe kwa kuing'oa Al Merrikh ya Sudan kwa ushindi wa jumla wa mabao 3-0, huku Clement Mzize akiandika rekodi ya kuifunga nje ndani Wasudani na kuivusha timu hiyo.
Mzize alifunga moja ya mabao mawili yaliyoizamisha Al Merrikh kwenye uwanja wa nyumbani wa Kigali Pele, jijini Kigali na leo ametupia tena baada ya wageni kuibana Yanga kwa mjuda mrefu wa mchezo huo.