PETRO de Luanda ya Angola leo imeitibulia rekodi TP Mazembe baada ya kutoa suluhu katika mchezo wa kwanza wa robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika uliopigwa mjini Lubumbashi, DR Congo.
Katika mchezo huo ambao Mazembe ilikuwa nyumbani na kulazimisha sare, timu hiyo ilimiliki mpira kwa asilimia 60 dhidi ya 40 za Petro, lakini hadi mwisho hakukuwa na mbabe.