Klabu ya Simba itamkosa mshambuliaji wake, Moses Phiri kwa wiki moja hadi mbili kutokana na jeraha alilopata katika mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya Kagera Sugar.
Phiri amekuwa mchezaji tegemeo katika kikosi cha Simba katika michezo 17 ya ligi amefanikiwa kufunga mabao 10 akiwa ndio kinara kikosini hapo na wa pili katika ligi akizidiwa na Fiston Mayele (Yanga) 13.