EWAAA...ndivyo walivyosikika mashabiki wa soka walioujaza Uwanja wa Azam Complex, jijini Dar es Salaam, baada ya Simba kulazimishwa sare nyumbani na Power Dynamos ya Zambia na kukata tiketi ya kutinga makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika ikiifuata Yanga iliyotangulia mapema.
Sare hiyo imeinufaisha Simba kufuzu hatua hiyo kwa kutumia kanuni ya faida ya bao la ugenini baada ya awali kutoka sare ya 2-2 ugenini wiki mbili zilizopita zilipokutana kwenye Uwanja wa Levy Mwanawasa, mjini Ndola kwa matokeo ya jumla kuwa sare ya 3-3 na kufanya iwe mara ya sita kwa timu hiyo kucheza hatua hiyo kwa michuano ya CAF.
Mbali na kufuzu hatua hiyo, Simba pia imejihakikishia kukunja Dola 700,000 (zaidi ya Sh 1.8 Bilioni) ikiungana na wababe wengine waliofuzu mapema wikiendi iliyopita