Mshambuliaji Moses Phiri ameiweka Simba pazuri ikiendeleza rekodi ya kutopoteza mechi za Ligi Kuu Bara ikiifunga Ihefu FC mabao 2-1 katika mchezo uliochezwa Uwanja wa Benjamin Mkapa.
Mabao ya mchezo huo yamefungwa na Jean Baleke dakika ya 13, Moses Phiri (65) kwa Simba na Ismail Mgunda dakika ya 25 akifunga bao pekee kwa Ihefu.
Huu ulikuwa mchezo wa sita kwenye Ligi Kuu Bara kwa Simba, ikiwa imefanikiwa kushinda yote na kukusanya pointi 18, ikiwa ndiyo timu pekee iliyofanikiwa kufanya hivyo kwenye ligi hadi sasa.