KOCHA Mkuu wa Simba, Abdelhak Benchikha hataki utani, kwani baada ya kukiangalia kikosi hicho alichoanza kukifundisha wiki mbili zilizopita amebaini anahitaji kiungo ‘mkata umeme’ wa kusaidia kuifanya timu kuwa na muunganiko mzuri eneo la kati hadi mbele na fasta akatoa jina la mido fundi kutoka Chad.
Nyota huyo amekuwa akihusishwa na Simba tangu msimu uliopita, lakini dili lilikwama na sasa ikiwa chini ya Kocha Abdelhak Benchikha aliyewahi kufanya naye kazi RS Berkane ya Morocco imemuita mezani ili kufanya mipango ya kumsajili kupitia dirisha dogo linalofunguliwa kesho.