Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Adebayor mambo freshi Singida Black Stars

Muktasari:

  • Adebayor aliyejiunga na timu hiyo msimu huu akitokea AS GNN ya kwao Niger aliyojiunga nayo Januari mwaka huu kwa mkopo akitoka AmaZulu FC ya Afrika Kusini, hajacheza mchezo wowote ndani ya kikosi hicho baada ya kupewa programu maalumu.

KOCHA Mkuu wa Singida Black Stars, Patrick Aussems amesema kwa sasa nyota mpya wa kikosi hicho, Victorien Adebayor yupo tayari kuanza kuitumikia timu hiyo baada ya awali kumpa programu zake maalumu kwa ajili ya kujiweka fiti kikosini humo.

Adebayor aliyejiunga na timu hiyo msimu huu akitokea AS GNN ya kwao Niger aliyojiunga nayo Januari mwaka huu kwa mkopo akitoka AmaZulu FC ya Afrika Kusini, hajacheza mchezo wowote ndani ya kikosi hicho baada ya kupewa programu maalumu.

"Adebayor alihitaji muda zaidi kwa sababu alichelewa kujiunga na wenzake kutokana na changamoto za kifamilia, ilibidi abaki Singida kwanza na tunashukuru maendeleo yake kwa sasa ni mazuri na yupo tayari kucheza kikosini," alisema Aussems.

Aussems aliongeza, Adebayor atajiunga na mazoezi ya moja kwa moja na mwenzake waliowasili jana mjini Singida na atakuwa sehemu ya kikosi kitakachohusika katika mchezo ujao wa timu hiyo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya JKT Tanzania Septemba 29.

Singida imerejea mjini Singida ikitokea Mwanza ilipoibuka na ushindi wa bao 1-0, dhidi ya Pamba Jiji na kuifanya timu hiyo kuendelea kusalia kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu Bara baada ya kufikisha jumla ya pointi 12 katika michezo minne.

Uwepo wa nyota huyo unaongeza machaguo mengi kwa Aussems kutokana na Adebayor kucheza katika wingi zote mbili kwa ufasaha kwa maana ya kulia na kushoto huku akicheza pia kama mshambuliaji wa kati, eneo waliopo mastaa, Elvis Rupia na Joseph Guede.