Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Fei Toto amkingia kifua Prince Dube

Muktasari:

  • Licha ya kumtetea kukosa nafasi humtokea yeyote uwanjani, lakini akaenda mbali kwa kumtabiria makubwa nyota huyo wa kimataifa wa Zimbabwe, atafanya makubwa Yanga tofauti na watu wanavyomchukulia kwa sasa.

KIKOSI cha Yanga jana usiku kilikuwa uwanjani kurudiana na CBE SA ya Ethiopia katika mechi ya raundi ya pili ya Ligi ya Mabingwa Afrika, huku mashabiki wakiwa bado wanamuota Prince Dube kwa kitendo cha kupoteza nafasi nyingi kwenye mchezo wa kwanza ugenini, sasa kiungo mshambuliaji wa zamani wa timu hiyo anayekipiga Azam FC, Feisal Salum ‘Fei Toto’ ameibuka na kumkingia kifua nyota huyo.

Licha ya kumtetea kukosa nafasi humtokea yeyote uwanjani, lakini akaenda mbali kwa kumtabiria makubwa nyota huyo wa kimataifa wa Zimbabwe, atafanya makubwa Yanga tofauti na watu wanavyomchukulia kwa sasa.

Fei Toto amecheza timu moja Dube Azam kabla ya kutimka na kujiunga na Yanga msimu huu katika usajili ulijaa mizengwe kama ilivyokuwa kwake wakati anaondoka Yanga kwenda Chamazi na Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan kuingilia kati alipoialika Yanga Ikulu kuipongeza kwa kufika fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika msimu wa 2022-2023.

Akizungumza na Mwanaspoti, Fei Toto alisema Dube ni mshambuliaji mzuri na ana jicho la kuona lango, kwa suala la kufunga hasa katika kikosi alichopo sasa anamwona akifanya vizuri kutokana na kuzungukwa na wachezaji wengi wenye uwezo mkubwa.

“Dube ni mchezaji mzuri, mbali na kufunga ana uwezo mzuri wa kutengeneza nafasi. Nimefanya naye kazi japo ni kwa muda mchache, lakini nimeona ubora alionao, naamini Yanga atafanya mambo makubwa,” alisema Fei Toto na kuongeza;

“Suala la kukosa ni sehemu ya mchezo. Sio rahisi kama wengi wanavyoamini anakosa nafasi za wazi, Yanga hawajafanya makosa kumsajili ataongeza kitu na anatakiwa kupewa muda,” alisema Fei Toto na kuongeza wao bado ni marafiki na wanawasiliana licha ya kucheza timu tofauti.

“Soka ni furaha siwezi kushindwa kuwasiliana na wachezaji wenzangu kutokana na upinzani wa timu, kuna maisha nje ya soka. Nawasiliana na wachezaji wote ambao nimekuwa karibu nao nje ya upinzani wa soka,” alisema Mchezaji Bora huyo wa Kombe la Shirikisho na aliyemaliza na mabao 19 Ligi Kuu Bara nyuma ya Stephane Aziz Ki wa Yanga.

“Nimecheza Yanga kuna marafiki zangu, Simba kuna marafiki zangu sio timu hizo tu timu zote za ligi kuna wachezaji tunawasiliana, ndiyo itakuwa Dube ambaye ni miezi tu tumetoka kucheza timu moja,” alisema Fei aliyesisitiza mbali na urafiki wao pia alikuwa anafurahi kucheza pamoja na Dube aliyekiri wakati anaondoka alikuwa tayari wametengeneza pacha nzuri ya maelewano Azam iliyomaliza nafasi ya pili Bara.