Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kriketi T20: Tanzania yailiza Mali, Ghana Malawi safi

T20 Pict
T20 Pict

Muktasari:

  • Mali wakiwa ni wageni kabisa katika mchezo  wa kriketi ndiyo walioanza kubeti na kufanikiwa kutengeneza mikimbio  18 tu baada ya wote 10 kutolewa wakiwa wametumia mizunguko  12 kati ya 20 iliyowekwa.

INAWEZA ikaingia katika vitabu vya rekodi kama mechi rahisi kuliko zote Tanzania imewahi kushinda katika mchezo wa kriketi baada ya kuifunga Mali kwa wiketi 10 katika mchezo wa ufunguzi wa michuano ya kufuzu kombe la dunia kwa kriketi ya mizunguko 20 iliyopigwa katika uwanja wa Dar Gymkhana mwishoni mwa juma.

Mali wakiwa ni wageni kabisa katika mchezo  wa kriketi ndiyo walioanza kubeti na kufanikiwa kutengeneza mikimbio  18 tu baada ya wote 10 kutolewa wakiwa wametumia mizunguko  12 kati ya 20 iliyowekwa.

Tanzania iliweza kujibu vyema alama hizi dhaifu  kwa kutengeneza mikimbio 19 bila ya kupoteza wiketi ikiwa imetumia mizunguko  0.5 kati ya 20 na hivyo kuondoka ma ushindi wa wiketi zote 10.

Sanze Kamate  na Yacouba Konate  ndiyo walocheza vizuri kwa Mali baada kila mmoja wao kutengeneza mikimbio 3 tu.

Sanjay Bom  aliyeungusha  wiketi 4 za wapinzani,Laksh Snehal  na Harsheed Chohan  aliyepata wiketi 2, walichangia sana kuifanya Tanzania ishinde kirahisi  mchezo huo.

Katika mechi nyiongine ya ufunguzi, Ghana iliwafunga Cameroon kwa wiketi 8 katika mchezo uliopigwa katika uwanja UDSM jijini.

Cameroon ndiyo walioanza kubeti na kufanikiwa kutengeneza  mikimbio  40 baada ya wote 10 kutolewa  wakiwa wametumia mizunguko  14 kati ya 20.

Wakitumia mizunguko 8 tu, Ghana waliweza kuzifikia alama za wapinzani wao kwa kupata  mikimbio 41 huku wakipoteza wiketi 2 na hivyo kutakata na ushindi wa wiketi 8.

Kofi Bagabena aliyetengeneza mikimbio 10 na Vincent Ateak aliyeongezea mikimbio 9 walikuwa ni mssada mkubwa kwa ushindi wa Ghana katika mechi hiyo.

Mechi ya tatu kati ya Malawi na Lesotho ndiyo iliyoongoza kwa wingi wa mikimbio baada ya Malawi kuifunga Lesotho kwa mikimbio 92 katika uwanja wa UDSM.

Wakiwa wamepata kura ya kuanza, Malawi walifanikiwa kutengeneza mikimbio 144  baada ya kumaliza mizunguko yote 20 wakiwa wamepoteza wiketi 4.

Alama hizo zilikuwa ni mlima mrefu sana kwa Lesotho, kwani jitihada zao ziligota kwenye mikimbio   52 baada ya wote 10 kutolewa wakiwa wametumia mizunguko 14 kati ya 20, na hivyo kuwafanya Malawi  wajivune kwa ushindo mnono wa mikimbio 92.

Nyota wa mikimbio katika mechi hiyo alikuwa Sami Mohammad Sohail  wa Malawi  ambaye peke yake alitengeneza mikimbio 61.