Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mbio za magari sasa milima ya Uluguru

Muktasari:

  • Raundi ya tatu ya ubingwa wa mbio za magari kitaifa  itapigwa mkoani Morogoro tarehe 12 na 13 mwezi wa kumi  kiasi cha mwezi mmoja baada ya kukamilika kwa raundi  ya pili mkoani Iringa.

HIFADHI ya misitu ya Mkundi mkoani Morogoro itakuwa ndiyo shuhuda wa raundi ya tatu ya ubingwa wa mbio za magari kitaifa zitakazofanyika mkoani humo mwanzoni mwa mwezi Oktoba mwaka huu.

Raundi ya tatu ya ubingwa wa mbio za magari kitaifa  itapigwa mkoani Morogoro tarehe 12 na 13 mwezi wa kumi  kiasi cha mwezi mmoja baada ya kukamilika kwa raundi  ya pili mkoani Iringa.

Klabu ya Mount Uluguru ndiyo waandaaji wa mbio hizi za  siku mbili ambazo kwa mujibu wa mwemyekiti wa klabu hiyo, Gwakisa Mahigi zinatarajiwa kushirikisha madereva  kutoka nchini na wachache kutoka nchi za Kenya, Uganda na Zambia.

“Maandalizi yamekwisha anza na yako katika hatua za mwisho huku mazungumzo na wadhamini yakiwa pia yamefikia katika hatua nzuri,” alisema Mwenyekiti huyo wa klanu ya Mount Uluguru.

Kwa mujibu wa Mahigi, madereva wanaotarajiwa kushiriki wanatoka mikoa ya Arusha, Dar es Salaam, Iringa, Kilimanjaro,Tanga na Morogoro ambao mshiriki  wake Waleed Nahdi alikuwa wa kuanza kuthibitisha ushiriki wake.

Baada ya kupata pointi 16  za kwanza katika raundi ya pili ya mbio za ubingwa wa magari kitaifa mkoani Iringa, dereva huyu chipukizi ameahidi kufanya makubwa katika  raundi ya tatu  ambayo amedai inachezwa nyumbani kwake.

“Nataka niwathibishie wapenzi wangu na wana Morogoro wote kwamba sasa nimekomaa kimchezo na nawaahidi kufanya makubwa katika raundi hii,” alisema Nahdi ambaye  huendesha gari aina ya Subaru Impreza N10.

Raundi ya tatu inategemewa kutoa muangaza wa nani anastahili kuutwaa ubingwa wa mbio za magari kitaifa kati ya madereva kutoka  Dar es Salaam na wale kutoka Arusha.

Kuelekea mbio za raundi ya tatu, Manveer Birdi wa Dar es Salaam  ndiye anayeongoza kwa pointi akifuatiwa na Gurpal Sandhu wa Arusha na Randeep Birdi wa Dar es Salaam.

“Naamini nitaurudia tena uongozi baada ya kushindwa kumaliza mbio za magari za Iringa kutokana na gari yangu kupata hitilafu katika hatua za mwishoni kabisa,” alisema Randeep Birdi ambaye aliukwaa uongozi baada ya kushinda raundi ya kwanza mjini Tanga.

Kuna raundi tano mwaka huu ili kukamalisha kalenda ya mbio za magari kwa msimu huu.