Tabora yajipanga kuinua wasichana
Muktasari:
- Alisema kabla ya kuanza mwaka huo, wanakusudia kuanda mafunzo ya mchezo wa kikapu ya mara kwa mara katika shule za msingi, sekondari pamoja ns vyuo.
KATIBU mkuu wa Chama cha Mpira wa Kikapu Tabora, Emanuel Wama amesema mkakati walioweka kwa mwaka 2025, ni kuhakikisha wanakuwa na wachezaji wengi wa kike.
Alisema kabla ya kuanza mwaka huo, wanakusudia kuanda mafunzo ya mchezo wa kikapu ya mara kwa mara katika shule za msingi, sekondari pamoja ns vyuo.
“Kwa kweli tumejipanga pia kuandaa mabonanza kwa ajili ya kuhamasisha wasichana waweze kujitokeza,” alisema Wama na kuongeza, wamejipanga kushirikiana na wahalimu na wafanyakazi kuhamasisha watoto wa kike kujitokeza.
Wakati huohuo, timu ya Zenga Hawks iliifunga Urambo Sixers kwa pointi 56-45, katika ligi ya kikapu ya Tabora iliyofanyika kwenye uwanja J.J Mkuda Spot Complex.
Katika mchezo huo, Urambo iliongoza robo ya kwanza kwa pointi 9-7, robo ya pili Zenga Sixers ikaongoza kwa pointi 11-8, 22-15 na 16-13.
Katika mchezo mwingine uliochezwa uwanjani hapo, Mboka Kings iliifunga U.S.S Wolves kwa pointi 62-35.