Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kwa Joh Makini hakuna mwingine kama Jide

Muktasari:

  • Joh Makini ametoa albamu, kushinda Tuzo za Muziki Tanzania (TMA), kushiriki katika miradi mikubwa ya muziki ya kimataifa pamoja kushirikiana na wasanii wa huko kitu kinachomfanya kuendelea kuwepo. Fahamu zaidi. 

KABLA ya Joh Makini alitumia jina la Rapcha, na sasa ni miaka 18 tangu ametoka rasmi kimuziki na bado anaendelea kuwahudumia mashabiki wake kwa nyimbo kali za rap na maonyesho ya hapa na pale.

Joh Makini ametoa albamu, kushinda Tuzo za Muziki Tanzania (TMA), kushiriki katika miradi mikubwa ya muziki ya kimataifa pamoja kushirikiana na wasanii wa huko kitu kinachomfanya kuendelea kuwepo. Fahamu zaidi. 


1. Joh Makini alianza muziki katika kundi la River Camp mkoani Arusha, alitoka kimuziki na wimbo wake, Chochote Popote (2006) ambao ulijumuishwa katika albamu yake ya kwanza, Zamu Yangu (2007).


2. Wimbo huo uliotengenezwa na Dunga wa Madungu Digital, unatajwa katika orodha ya nyimbo kali za Hip Hop zinazozungumzia mapenzi. Nyingine ni ‘Mamsapu’ wa Hard Blasters Crew (HBC), ‘Hayakuwa Mapenzi’ wa Sugu na ‘Zali la Mentali’ wa Professor Jay.


3. Tuzo ya kwanza kushinda Joh Makini ni kutoa TMA kama Msanii Bora wa Hip Hop 2012, kisha kundi lake la Weusi kupitia wimbo wao, Gere (2013) likaja kushinda tuzo hizo mbili kwa mpigo kama Wimbo Bora wa Hip Hop na Kundi Bora la Mwaka 2014. 


4. Kolabo ya Joh Makini na Chidinma kutoka Nigeria, Perfect Comb (2016) ilikuja baada ya kukutana Nairobi, Kenya kwenye msimu wa nne wa Coke Studio Africa 2016 ambapo walishirikiana kutumbuiza wimbo wake, Nikumbatie (2013).

Na hadi sasa huo ndio wimbo wa Joh Makini ambao video yake imetazamwa zaidi YouTube kwa muda wote ikiwa na ‘views’ zaidi ya milioni 1.8 tangu utoke miaka saba iliyopita.


5. Video ya wimbo wa Joh Makini, Sijutii (2012) iliyofanyika Arusha ndiyo ilimtangaza zaidi Director Nisher na kuanza kumpa kazi za wasanii mbalimbali hasa wa Bongofleva. Nisher aliyefariki mwaka uliopita alikuja kufanya video nyingine ya Joh Makini, XO (2014).


6. Licha ya kufanya kazi na wasanii wa kimataifa kama Davido, AKA, Chidinma, Navio n.k, Joh Makini ana nyimbo na wakali wengine kama Fallz, Y Cee na Cassper Nyovest ambazo bado hazijatoka.


7. Kundi la Weusi lilizaliwa kufuatia kuvunjika kundi la Nako 2 Nako, hivyo G Nako na Lord Eyes wakajiunga na Nikki wa Pili, Joh Makini na Bonta ambao nao walitokea kundi la River Camp, kisha wakanzisha Weusi.


8. Hadi sasa Weusi wamefanikiwa kutoa wimbo mmoja pekee ambao umekutanisha wasanii wote watano wa kundi hilo, wimbo huo, Watoto wa Mungu (2013) ilitoka chini ya Bongo Records kwa P-Funk Majani.


9. Lady Jaydee ndiye msanii wa kike Bongo ambaye Joh Makini kafanya naye kolabo nyingi, wawili hao wameshirikiana katika nyimbo tatu, Kilimanjaro (2011), Ni Hapo (2020) na Kiwembe (2020) ambao ulirekodiwa miaka mingi nyuma kabla ya kutoka.


10. Tangu mwaka 2020 hadi 2024, hakuna mwaka uliopita bila Joh Makini kutoa wimbo wa mapenzi, alianza na Dangerous (2020) ft. Nahreel, Swagg (2021) ft. Nandy, Tanzanite (2022) ft. Jay Rox, Bobea (2023) na Formula (Moto Zimelia) (2024).

Nyimbo zake nyingine za aina hiyo ni kama Sitochoka (2007) ft. Farida, Nikumbatie (2013) ft. Fundi Samweli, XO (2014) ft. G Nako, Unanichora (2014) ft. Ben Pol, Waya (2017), Mipaka (2017), Kiwembe (2020) ft. Lady Jaydee, Too Much (2023) ft. Damian Soul na kadhalika.