Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ninja nje wiki moja, akosa Kombe la Shirikisho

Ninja Pict
Ninja Pict

Muktasari:

  • Beki huyo wa zamani wa Yanga kwenye mkondo wa kwanza hakuwepo kwenye kikosi hicho kilichopoteza mchezo dhidi ya Bravos do Maquis ya Angola kwa bao 1-0 kutokana na jeraha la goti.

BEKI wa FC Lupopo ya Congo, Abdallah Shaibu 'Ninja' amesema atakuwa nje kwa wiki moja akiukosa mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Bravos ya Angola.

Beki huyo wa zamani wa Yanga kwenye mkondo wa kwanza hakuwepo kwenye kikosi hicho kilichopoteza mchezo dhidi ya Bravos do Maquis ya Angola kwa bao 1-0 kutokana na jeraha la goti.

Akizungumza na Nje ya Bongo, Ninja alisema kwa mujibu wa daktari anaweza kukaa nje ya uwanja kwa wiki moja kisha akarudi kutokana na udogo wa jeraha lake.

Aliongeza, wiki iliyopita alifanya mazoezi ya Gym na sasa anafanya ya uwanjani hivyo atakosa mechi ya marudiano lakini akiziwahi nyingine za ligi.

"Ndiyo nimeanza mazoezi ya uwanjani na daktari kaniambia naweza kurudi uwanjani baada ya wiki moja, hivyo tunaendelea kupambana," alisema Ninja.

Baada ya kumalizana na michezo ya kimataifa, Lupopo itaanza ligi ikivaana na Makiso Septemba 29 na huenda Ninja akawa sehemu ya kikosi hicho.