Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

TBF yalamba Sh194 milioni BetPawa

Muktasari:

  • Ofisa Mkuu wa Biashara wa BetPawa na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Mchezo huo, Ntoudi Mouyelo alisema wameamua kudhamini mpira wa kikapu nchini ili kusaidia kuukuza mchezo huo ambapo Sh130 milioni zimetengwa kwa ajili ya Locker Room Bonus na Sh14 milioni kwa zawadi za ushindi na fedha zinazobaki zitasaidia usimamizi wa TBF.

KAMPUNI ya michezo ya kubashiri ya BetPawa imetangaza udhamini wa Sh194.8 milioni kwa ajili ya Ligi ya Taifa ya Mpira wa Kikapu (NBL) inayoendeshwa na Shirikisho la Mpira wa Kikapu Tanzania (TBF) ambayo inafanyika mjini Dodoma.

Ofisa Mkuu wa Biashara wa BetPawa na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Mchezo huo, Ntoudi Mouyelo alisema wameamua kudhamini mpira wa kikapu nchini ili kusaidia kuukuza mchezo huo ambapo Sh130 milioni zimetengwa kwa ajili ya Locker Room Bonus na Sh14 milioni kwa zawadi za ushindi na fedha zinazobaki zitasaidia usimamizi wa TBF.

“Kampuni yetu imejizatiti katika kukuza mchezo pamoja na kusaidia jamii,” alibainisha Mouyelo huku akifafanua kwamba “Locker Room Bonus” katika NBL, ni mfumo wa zawadi kwa wachezaji 12 na maafisa wanne wa timu inayoshinda watakabidhiwa Sh140,000 kila mmoja.

Mbali na Locker Room Bonuses, BetPawa imejitolea Sh14 milioni kugawanywa kwa wachezaji bora na timu itakayoshinda mwishoni mwa msimu wa 2025 huku kampuni hiyo ikiahidi kuwasadia mabingwa wa NBL katika Ligi ya Mpira wa Kikapu ya Afrika inayofuata.

“Tunalenga kuukuza mpira wa kikapu katika kanda hii kama tulivyofanya Rwanda kupitia ushirikiano kama huu na Ferwaba (Shirikisho la Mpira wa Kikapu Rwanda),” alisema.

Akizungumza kwa niaba ya Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa, na Michezo, Hamisi Mwinjuma, Kaimu Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo, Tamba Boniface alisema udhamini huo unaonyesha imani ya kampuni hiyo kwa vipaji, uwezo na mustakabali wa kikapu nchini Tanzania.