Dias: Wenzetu wanatuombea tushuke
Muktasari:
- Man City ambayo imepoteza mechi nne mfululizo katika mashindano yote huku mchezo wa mwisho wakichapwa na Brighton, Jumamosi iliyopita kwa mabao 2-1. Kwa sasa ndio mabingwa watetezi wa EPL wakiwa wameshinda mara nne mfululizo.
MANCHESTER, ENGLAND: BEKI wa Manchestr City, Ruben Dias amesema timu nyingi zinawaombea mabaya na kutaka wapoteze, lakini timu yake ilivuka salama na kushinda tena taji la Ligi Kuu England (EPL) msimu huu.
Man City ambayo imepoteza mechi nne mfululizo katika mashindano yote huku mchezo wa mwisho wakichapwa na Brighton, Jumamosi iliyopita kwa mabao 2-1. Kwa sasa ndio mabingwa watetezi wa EPL wakiwa wameshinda mara nne mfululizo.
Akizungumza na BBC, Dias alisema: “Ni kawaida kuwa na nyakati kama hizi hasa kwa sababu watu wengi wanataka kutuangusha na wanaombea waone tunaanguka. Tunakubaliana na hali hii na tunachukua kama sehemu ya changamoto ndio maana tunapenda sana kupambana. Isingekuwa changamoto kama hizi inawezekana tusingekuwa na mafanikio haya. Haya ni maisha yetu ya kila siku na tutaendelea kupambana.”
Beki huyo pia alisisitiza kwamba ni mapema sana kuanza kusema kwamba wameshapoteza ubingwa kwani msimu unaendelea na kuna mengi yanayoweza kutokea.
“Bado ni mapema katika msimu na kuna mengi yatakayojiri. Sote tunajua jinsi Ligi Kuu ilivyo. Ndiyo maana tunapenda sana hizi changamoto na naamini huu utakuwa ni msimu wa kipekee.”
Man City imepoteza mechi nne za michuano yote mwaka huu kwa mara ya kwanza tangu mwaka 2006 na ilikuwa mara ya kwanza kwa kocha wao Pep Guardiola kupata kipigo cha mechi nne mfululizo katika kipindi chote cha uongozi wake.
Baada ya kupoteza dhidi ya Bournemouth, Tottenham Hotspur, Sporting CP na sasa Brighton, vijana hao wa Guardiola wanatarajia kushuka tena uwanjani kuendelea kuweka hai matumaini ya kuchukua ubingwa msimu huu Novemba 23 watakapokutana na Tottenham.