Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Jokic, Garland watakata NBA mapema na rekodi

Muktasari:

  • Jokic ametwaa tuzo hiyo kutokana na maajabu aliyoyafanya katika ligi hiyo ndefu kutoka Kanda ya Magharibi, huku Garland akitwaa kwa Kanda ya Mashariki.

WASHINGTON, MAREKANI: NYOTA wa kiungo wa Denver Nuggets, Nikola Jokic na mlinzi wa Cleveland Cavaliers, Darius Garland wameuanza vyema msimu mpya wa Ligi ya Kikapu Marekani (NBA), baada ya kutangazwa kubeba tuzo ya mchezaji bora wa wiki ya pili ya mashindano hayo.

Jokic ametwaa tuzo hiyo kutokana na maajabu aliyoyafanya katika ligi hiyo ndefu kutoka Kanda ya Magharibi, huku Garland akitwaa kwa Kanda ya Mashariki.

Jokic aliiongoza Nuggets kupata rekodi ya ushindi 4-0 katika wiki ya Novemba 4-10, akiwa na wastani wa kushangaza wa pointi 29.5, ribaundi 15.8 na asisti 14.5 kwa kila mchezo.

Nyota huyo pia alikuwa na ‘triple-doubles’ katika michezo yote minne na kurekodi asilimia za mitupo 566/.500/.897 katika ushindi dhidi ya Toronto, Oklahoma City, Miami Heat na Dallas Mavericks.

Baada ya kuanza msimu kwa kusuasua, Denver sasa ina mfululizo wa ushindi wa michezo mitano na inashika nafasi nne za juu Magharibi ikiwa na rekodi ya 7-3.

Jokic ana wastani wa msimu wa pointi 29.7, ribaundi 13.7 na asisti 11.7 kwa kila mchezo, akishinda tuzo ya MVP kwa mara ya nne, huku akiongoza ligi kwa wastani wa ribaundi na asisti kwa kila mchezo.

Cavaliers, kwa upande mwingine pia walikuwa na wiki nzuri wakizishinda Milwaukee Bucks, New Orleans Pelicans, Golden State Warriors na Brooklyn Nets na kufikisha rekodi ya 11-0.

Garland ambaye anafurahia msimu wa mafanikio baada ya uliopita uliokuwa na mambo mengi, aliongoza kwa wastani wa pointi 25.0 na asisti 7.3 kwa kila mchezo na asilimia bora za mitupo .617/.576/.875.

Garland ni mlinzi wa pili wa Cleveland Cavaliers kutajwa kuwa mchezaji bora wa wiki wa Mashariki msimu huu baada ya Donovan Mitchell aliyetwaa tuzo hiyo Jumatatu iliyopita.

Katika kinyang’anyiro, Jokic alimshinda Anthony Davis, LeBron James, Anthony Edwards, Shai Gilgeous-Alexander, Kyrie Irving na Norman Powell kwa tuzo hiyo Magharibi.  Ilhali Garland alibeba Mashariki akiwashinda LaMelo Ball, Cade Cunningham, Bennedict Mathurin, Myles Turner, Jayson Tatum na Franz Wagner.