Kudus anukia Arsenal dirisha lijalo Ulaya
Muktasari:
- Kudus mwenye umro wa miaka 24, mkataba wake wa sasa unatarajiwa kumalizika mwaka 2028. Amezivutia timu nyingi kutokana na kiwango bora alichoonyesha tangu atue West Ham.
ARSENAL ipo tayari kulipa Pauni 83 milioni kwenda West Ham United kwa ajili ya kumsajili kiungo wa timu hiyo na timu ya taifa ya Ghana, Mohammed Kudus katika dirisha la Januari, 2025.
Kudus mwenye umro wa miaka 24, mkataba wake wa sasa unatarajiwa kumalizika mwaka 2028. Amezivutia timu nyingi kutokana na kiwango bora alichoonyesha tangu atue West Ham.
Tangu kunza kwa msimu huu Kudus amecheza mechi 20 za michuano yote, amefunga mabao manne na kutoa asisti mbili.
Kabla ya kujiunga na West Ham staa huyu alikuwa akihusishwa na timu nyingi za England ambazo zilivutiwa na kiwango chake katika michuano ya Kombe la Dunia 2022.
Kocha wa Arsenal, Mikel Arteta anataka kuboresha eneo la ushambuliaji kutokana na upungufu ambao upo kwa sasa.
Joshua Zirkzee
MANCHESTER United inataka kumtoa kwa mkopo straika wake raia wa Uholanzi, Joshua Zirkzee katika dirisha la majira baridi mwakani kwenda Italia ambako timu kibao zimeonyesha nia ya kumtaka kumsajili. Mabosi wa Man United wanataka kumwachia kwa mkopo wakiwa na matumaini kwamba atakwenda kupata nafasi ya kucheza jambo linaloweza kumrudisha katika ubora wake.
Jonathan David
JUVENTUS inadaiwa kuwa ndio timu inayoongoza katika mchakato wa kumsajili straika wa Lille na timu ya taifa ya Canada, Jonathan David, 24, katika dirisha lijalo la majira ya baridi. Nyota huyo pia anawindwa sana na Manchester United, Liverpool na Inter Milan ingawa zina asilimia chache zza kumpata. Mkataba wa David unatarajiwa kumalizika mwisho wa msimu huu.
Mike Maignan
BENCHI la ufundi la Manchester City linamtazama kwa makini kipa wa AC Milan, Mfaransa Mike Maignan linayeweza kumsajili katika dirisha lijalo la majira ya kiangazi ili kuziba pengo la Ederson ambaye anahusishwa kuwa katika rada za timu za Saudi Arabia. Maignan mwenye umri wa miaka 29, mkataba wake na Milan unatarajiwa kumalizika 2026.
Jobe Bellingham
MASKAUTI wa Borussia Dortmund wanadaiwa kuwepo England ambapo wanamtazama kiungo wa Sunderland, Jobe Bellingham, 19, na wameridhishwa na kiwango chake hivyo wanataka kumsajili dirisha la majira ya baridi mwakani. Jobe ni mchezaji tegemeo kikosi cha kwanza Sunderland na msimu huu amecheza mara 11 na kufunga mabao mawili.
Sergio Ramos
MPANGO wa beki Sergio Ramos kujiunga na Real Madrid katika dirisha lijalo unadaiwa kukwama na sasa timu hiyo inaangalia uwezekano wa kumsajili beki wa Bayer Leverkusen, Jonathan Tah ambaye mkataba wake unatarajiwa kumalizika mwisho wa msimu huu, lakini yenyewe inataka kumchukua Januari. Real Madrid imekuwa ikihangaika kusajili beki baada ya kuumia kwa Eder Miltao.
Leroy Sane
WWINGA wa Bayern Munich na timu ya taifa ya Ujerumani, Leroy Sane yupo katika mazungumzo na wawakilishi timu hiyo kwa ajili ya kuongeza mkataba mpya baada ya kuona kuna timu nyingi zinazohitaji huduma yake. Sane mwenye umri wa miaka 28, amekuwa akihusishwa na timu ya Barcelona baada ya msimu huu kumalizika.
Paul Pogba
KIUNGO wa kimataifa wa Ufaransa, Paul Pogba, 31, yupo katika hatua za mwisho kufikia makubaliano Juventus kwa ajili ya kuvunja mkataba wake ili kujiunga na timu anayotaka mwakani. Pogba anarejea uwanjani Machi baada ya kumaliza kifungo cha miezi 18 kutokana kukutwa na hatia ya matumizi ya dawa zilizopigwa marufuku michezoni.Rum sum soloremolut int verovite la cori