Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ruud van sasa atajwa Burnley

Vann Pict
Vann Pict

Muktasari:

  • Ruud Van raia wa Uholanzi aliachana na Man United hivi karibuni baada ya kocha aliyetua klabuni hapo Ruben Amorim, kusema kuwa anataka kufanya kazi na wasaidizi wake na siyo wale waliopo klabu hapo.

MANCHESTER, ENGLAND: BAADA ya kuiongoza Man United kwenye michezo minne aliyekuwa kocha wa timu hiyo wa muda Ruud Van Nistrelrooy anatajwa kuwaniwa na timu ya Championship.

Ruud Van raia wa Uholanzi aliachana na Man United hivi karibuni baada ya kocha aliyetua klabuni hapo Ruben Amorim, kusema kuwa anataka kufanya kazi na wasaidizi wake na siyo wale waliopo klabu hapo.

Maamuzi hayo yalitokea pamoja na kwamba Van Nistelrooy ambaye alikuwa kocha wa muda baada ya kuondolewa kwa Erik ten Hag alishinda michezo mitatu na kutoka sare mmoja kwenye kipindi chake kifupi kwenye timu hiyo.

Sasa tetesi zinaonyesha kuwa mshambuliaji huyo wa zamani wa Manchester United anatakiwa na kikosi cha Burnley ambacho awali kilikuwa kikifundishwa na Vincent Kompany ambaye kwa sasa yupo na Bayern Munich.

Hata hivyo, taarifa za awali zinasema kuwa kabla ya kutua Man United kuwa msaidizi wa Ten Hag, timu hiyo pia ilimtaka Van Nistelrooy ambaye aliamua kujiunga na United.

Sasa timu hiyo inataka kujaribu tena bahati yake ya kumchukua kocha huyo wa zamani wa PSV baada ya kuondoka United akiwa na rekodi nzuri.

Burnley baada ya kumkosa Ruud Van ilimchukua Scott Parker ambaye kwa sasa ameiongoza timu hiyo kwenye michezo 15 ya Championship akiwa ameshinda saba, kutoa sare sita na kupoteza mmoja timu yake ipo katika nafasi ya nne kwenye msimamo, tofauti ya pointi nne dhidi ya Sunderland iliyopo kileleni.

Hata hivyo, kuna hofu kama Burnley wanaweza wasifanye hivyo kwa sasa kwa kuwa mmiliki wa timu hiyo Alan Pace, amekuwa akiheshimika kwa kuwapa makocha muda hata kama timu hiyo inafanya vibaya kama alivyofanya kwa Sean Dyche na Vincent Kompany.