Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Tyson, Paul hatihati kuzichapa

Muktasari:


  • Pambano hilo lilipangwa kufanyika Jumamosi asubuhi kw asaa za afrika mashariki, katika Ukumbi wa AT&T, Arlington, Texas, Marekani.

TEXAS, MAREKANI: LILE pambano kali linalosubiriwa kwa hamu kati ya nguli wa mchezo huo, Mike Iron Tyson dhidi ya Jake Paul, huenda likasitishwa kutokana na tatizo la kiafya lililomkumba bingwa huyo wa zamani wa dunia uzito wa juu.

Pambano hilo lilipangwa kufanyika Jumamosi asubuhi kw asaa za afrika mashariki, katika Ukumbi wa AT&T, Arlington, Texas, Marekani.

Hadi Jumanne, mabondia wote walifanya mazoezi ya wazi pamoja na maandalizi mengine ya pambano hilo lakini huenda likaahirisha au kufutwa kabisa kutokana na kidonda cha chenye ukubwa wa inchi mbili na nusu kinachovuja damu alichokipata Tyson.

Hii inaweza ikawa mara ya pili kwa pambano hili kuahirishwa baada ya awali kupangwa kufanyika Julai, mwaka huu na liliahirishwa kutokana na sababu za kiafya za Tyson alizopata akiwa kwenye ndege.

Akisimulia tukio lake lililosababisha pambano la kwanza liahirishwe, Tyson alielezea: "Nilikwenda chooni 'katika ndege' na nikatema damu. Nilidondoka chini, nilikuwa natoa kinyesi kama mkaa. Nikamuuliza daktari, 'Nitaishi?' Na yeye hakusema hapana. Alisema kuna njia. Hapo ndipo nilipoanza kuwa na wasiwasi." 

Baadhi ya mashabiki wamekuwa na wasiwasi kuhusu afya ya Tyson, huku wmenyewe akijaribu kuwatoa hofu. Hata hivyo, inaelezwa, kabla ya pambano hilo Taasisi ya Boxing Kingdom itahitaji apitie vipimo viwili vya afya na ikishindikana pambano hilo litafutwa kabisa.

Inadaiwa Tyson alikubali kufanya vipimo hivyo miezi kadhaa iliyopita kama sehemu ya tahadhari za usalama na hivyo,  atalazimika kupita kwenye kipimo cha ubongo (EEG) na cha moyo (EKG) kabla ya kuruhusiwa kupanda ulingoni. Vipimo hivyo vilihitajika na Idara ya Leseni na Udhibiti ya Texas.