Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Vigogo Barca wataka maelezo kuhusu bao la Lewandowski

Muktasari:

  • Barcelona ilipoteza mechi ya pili katika Ligi Kuu Hispania (La Liga) msimu huu kwa kipigo cha 1-0 Jumapili, wiki iliyopita, lakini ilikosa bao baada ya mapitio ya VAR kubaini kwamba Lewandowski alifunga akiwa ameotea dakika ya 13.

BARCELONA, HISPANIA: VIGOGO wa Barcelona wameripotiwa kutuma barua kwenda kwa Shirikisho la Mpira wa Miguu Hispania, (RFEF) ili kupewa maelezo juu ya bao la Robert Lewandowski lililokataliwa dhidi ya Real Sociedad.

Barcelona ilipoteza mechi ya pili katika Ligi Kuu Hispania (La Liga) msimu huu kwa kipigo cha 1-0 Jumapili, wiki iliyopita, lakini ilikosa bao baada ya mapitio ya VAR kubaini kwamba Lewandowski alifunga akiwa ameotea dakika ya 13.

 Hata hivyo, viongozi wa Barcelona wanalalamika kuwa kulikuwa na kosa katika mfumo wa VAR, jambo lililosababisha waaamue kutuma barua ya kutaka maelezo.

Taarifa zinadai kwamba rais wa Barcelona, Joan Laporta alisikika akisema: “Haiwezekani kutokuwa bao.”

Kisha kocha Hans Flick alimwambia mwamuzi Cuadra Fernandez kuwa alifanya “uamuzi mbaya.”

Kupoteza kwa mechi kuliwafanya Barcelona wakose  fursa ya kuweka pengo la pointi tisa kileleni mwa La Liga dhidi ya wapinzani wao, Real Madrid.

Taarifa inaongeza kuwa Barcelona wanaomba maelezo ili kujua hasa kilichotokea na kujaribu kupata suluhu ili tukio kama hilo lisitokee tena.

Viongozi wa timu hiyo ambayo ni bingwa mara 27 wa La Liga walieleza kuwa video za marudio hazikuonyesha kama Lewandowski alikuwa ameotea, lakini VAR ilifanya kosa.

Barcelona inataka maelezo hayo kuwasilishwa kwao ndani ya wiki mbili za mapumziko ya kimataifa kabla haijarejea tena uwanjani kucheza dhidi ya Celta Vigo, Novemba 23 katika mchezo wa LaLiga.