Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Alikiba sasa aitamani Ufaransa

Muktasari:

  • Staa huyo anayetamba na nyimbo mbalimbali kama Utu, Mahaba, Mwana, Mapenzi yana Run Dunia, Sumu na nyingine, juzi usiku, alikuwa anashea mambo kadhaa na mashabiki akiwa live katika mtandao wa TikTok, ndipo alipoulizwa  kuhusiana na Ufaransa .

MSANII wa Bongo Fleva, Alikiba amesema laiti angekuwa anaweza kuzungumza lugha ya Kifaransa, angehamia Ufaransa kwa ajili ya kuishi, kutokana na kupenda nchi hiyo.

Staa huyo anayetamba na nyimbo mbalimbali kama Utu, Mahaba, Mwana, Mapenzi yana Run Dunia, Sumu na nyingine, juzi usiku, alikuwa anashea mambo kadhaa na mashabiki akiwa live katika mtandao wa TikTok, ndipo alipoulizwa  kuhusiana na Ufaransa .

“Ili niendelee kusalia Tanzania, nisijue kuzungumza Kifaransa, ukiachana na maneno machache ninayoweza kuongea ya hapa na pale. Katika nyimbo zangu nyingi, nimetumia maneno ya Kifaransa, kuonyesha ni jinsi gani napenda aina ya maisha yao, ndio maana nasema ningekuwa nimeishaijua lugha hiyo kitambo ningekuwa huko,” alisema staa huyo aliyewahi kucheza Ligi Kuu Bara akiwa na Coastal Union.

Wakati amejibu kuhusu Ufaransa, mwingine alimuuliza kama anaweza akaishi Jamaica, Alikiba hakuonyesha jibu lililonyooka zaidi ya kuishi kutamka Jamaica daah, kisha akaendelea na vaibu nyingine.

Vaibu la Kiba na mashabiki hao, lilikuwa kubwa huku wengine wakimtumia zawadi mbalimbali, kuonyesha namna gani wanafurahia kuzungumza naye live katika mtandao huo.

Kati ya mambo mengi aliyoyazungumza ni pamoja na  kumpongeza msanii Herry Sameer ‘Mr Blue’ kwa jinsi ambavyo ameendelea kufanya vizuri katika karia hiyo.

“Anafanya kazi nzuri tangu alipoanza kufanya muziki, si kazi rahisi kumentaini gemu, hivyo nampongeza Mr Blue kwa muziki mzuri anaoufanya,” alisema Kiba.