Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Anko lao ... Majibu Konki

Muktasari:

  • Jibu: Huyo aliyekwambia anaitaka figo yako nani? Usilazimishe ulemavu ilihali Mungu amekupa siha na afya tele. Ushauri wangu, tumia nguvu ulizonazo kufanya kazi ili upate mtaji wa biashara. Naamini ukichakarika bila kuchoka au kubagua kazi unatoboa freshi tu, kuliko hilo wazo la kiduwanzi. Hivyo tu, never give up!

1. ANKO Lao, kijana miaka 26, kusema kweli maisha yanabana mno na kuwa changamoto nyingi, kiasi nafikiria hata kuuza figo mmoja ili nipate pesa ya mtaji, nifanye biashara. Naomba ushauri wako.

Steven George, Ifakara

Jibu: Huyo aliyekwambia anaitaka figo yako nani? Usilazimishe ulemavu ilihali Mungu amekupa siha na afya tele. Ushauri wangu, tumia nguvu ulizonazo kufanya kazi ili upate mtaji wa biashara. Naamini ukichakarika bila kuchoka au kubagua kazi unatoboa freshi tu, kuliko hilo wazo la kiduwanzi. Hivyo tu, never give up!


2. ANKO Lao, kijana miaka 29, nimekuwa nikijitahidi kuonyesha upendo kwa kila nimpendaye, lakini wenzangu hawajawahi kunipenda kabisa na wala kujali. Hii inaweza kuwa ni kitu gani? Nisaidie.

Suleiman Salum,

Kariakoo

Jibu: Tafuta pesa upunguze malalamiko...kinachokuponza wewe, ni kuwa na fedha za mawazo, halafu unajibebisha kwa mademu wachungulia pochi wanaoamini upendo wameupata kwa mama zao. Ushauri wangu, tumia muda mwingi kupiga mishe, uzikusanye za kutosha...kisha tafuta saizi yako uoe. Hivyo tu!


3. ANKO Lao, binti miaka 22, kuna boy tunapendana, ila hajatulia kwani mara kadhaa nimemfuma na mademu na kuniomba msamaha, lakini habadiliki, nikimtaka tuachane anatishia kujiua. Nifanyeje?

Latifa Abdul, Tanga

Jibu: Kama kusoma hujui, basi hata picha nayo inakushinda? Hapo hakuna kitu, huyo jama’ako ni kimeo na ukimwendekeza ujue kabisa atakuua kwa presha kama sio kukuachia kijidudu. Mkwara wake wa kutaka kujiua ni gia tu, kwani amegundua umekufa na kuoza kwake. Sikufundishi kitu, uamuzi unao mwenyewe!


4. ANKO Lao, kijana miaka 31 dereva wa bodaboda, hapa kitaani kwetu kuna lishangazi limetokea kunipenda, ila nimesikia tetesi eti, ana mdudu na nimemtaka tukapime, lakini hataki. Nifanyeje?

Man Zuu, Kimara Dar

Jibu: Lishangazi la kazi gani wewe kama sio kutaka kujibebesha mzigo usio na sababu au we mario? Halafu, kama ushasikia bibie ana mdudu na hataki kupima hujiongezi tu! Iwapo ulishatambaa na chaki, wahi ukacheki afya...nawajua nyie bodaboda hampigwi mnacheza...ukiwa freshi, fanya chapu uoe ili utulie!


5. ANKO Lao, binti miaka 24, kuna mwanamume nampenda sana, lakini hajawahi kuniambia ananipenda. Nifanyeje ili ajue kama nampenda?

Amina Mussa, Dar

Jibu: We unachekesha kweli, yaani unakonda kwa mawazo kwa mtu asiye na mpango nawe wala kujua kama unampenda. Iwapo umemwelewa, jitahidi umfikishie ujumbe ujue, maana huenda anakonda kwa kumuwaza mtu aliye na jimbo na hesabu zake kwingine. Ukiona hajielewi, tafuta chake jingine maisha yaendelee!


6. ANKO Lao, kijana miaka 27, napambana na kazi za vibarua lakini nashindwa kupata pesa za mtaji, maana nikipata kazi siku mbili, nakaa homu wiki nzima bila ya kibarua. Natamani kuanzisha biashara yangu. Nifanyeje?

Pati Guju, Dodoma

Jibu: Tatizo lako umekariri maisha na kuamini hizo kazi za vibarua tu ndio za kukutoa, wakati kumbe ungeweza kupiga mishe nyingine kitaani ili uzichange za kutosha na kupata mtaji wa biashara unayoitaka. Ukiendelea kuishi kwa mazoea utachina na umri unazidi kusonga. Shauri yako!


7. ANKO Lao, binti miaka 25, kuna mtu tunapendana, ila alinitaka tukaishi wote, nikamtaka aende kwanza kujitambulisha kwa wazazi wangu, cha ajabu amenikatia mawasiliano kabisa. Nifanyeje nami nampenda?

Janeth Joseph, Mwanza

 Jibu: Hiyo njemba haina lolote, ilitaka kitonga tu kwako, kwani kama alikuwa anakupenda kitu gani kimemfanya azire...huyo anaonekana ni mtu wa visirani na kuzira ovyo, wakati wanaume hawasusi. Wee wala huna haja ya kupaniki, umeonyeshwa mapema rangi yake....Jitulize kwetu, atajitokeza tu wa kukuoa!


8. ANKO Lao, kijana miaka 28 kuna mwanamke tunapendana naye, ila tatizo kila siku ananilazimisha niende kikakae kwake, namini sina mzuka wa mambo hayo kabisa. Nifanyeje?

Juma Salum, Tanga

Jibu: Kula tano mwanangu, umefanya poa sana kumchomolea huyo manzi. Ukijiroga na kukubali kwenda kuishi kwake, ujue kabisa utadhalilika mbele ya safari. Hivi viumbe wanajijua wenyewe, kwani wakimchoka mtu wanatimua kama hawajawahi kumpenda. Komaa hivyo hivyo, ukifanya chapu mipango ya kuoana sasa!


9. ANKO Lao, nimeoa sasa ukiwa ni mwaka wa tano, ila mwenzangu anataka tukaishi kwao, nami sitaki. Nifanyeje.

Nembo Nembo, Iringa


Jibu: Ni kweli umeoa au unapiga deiwaka tu? Maana kama umeoa, sidhani kama mkeo anaweza kukupelekesha na mawazo wa kiduwanzi kama hayo, wakati anapaswa kukusikiliza kichwa cha familia...Ila nahisi mmebebana wangali wadogo, wakati akili hazijakomaa kujitegemea, ndo maana mnazingua!


10. ANKO Lao, binti miaka 25, nimeolewa ila hadi leo sijabahatika kupata mtoto. Nimetumia dawa mbalimbali na kwenda hospitali, ila mambo bado. Nifanyeje?

Salma, TMK Dar

Jibu: Pole sana, usikate tamaa. Ushauri wangu ni vyema ukaambatana na mumeo hospitalini ili mkapimwe nyote mjue nani mwenye tatizo, unaweza kusumbuka mwenyewe kumbe u mzima ila mwenzio ndio kimeo. Kama mtakuwa fiti nyote, zoeni kupiga shoo siku za hatari, kwani hata shamba huwa halilimwi hovyo tu!


11. ANKO Lao, kijana miaka 33, nina mchumba nimezaa naye mtoto mmoja, lakini kila nikimuambia amlete mwanangu hataki. Nifanyeje?

Marco, Dodoma

Jibu: Mayanki wa zama hizi mnazingua sana, yaani umemzalisha mwenzio kabla ya ndoa, halafu unataka kiulaini tu uletewe mtoto! Kwa nini usiende kwao kumjulia hali na kufanya haraka taratibu za kumuoa ili mumlee mtoto pamoja kama kweli unampenda? Unazingua ujue!


12. ANKO Lao, binti miaka 20 kuna boy tunapendana, ila siku hizi kabadilika sana kila nikimwambia kitu hanisikilizi na hata nikumtumia text hanijibu. Nifanyeje?

Tinah Tuner, Mwanza

Jibu: Kwa umri ulionao ungejikita kuitafuta kesho yako kuliko malavidavi, kuhusu huyo jama’ako huenda anaona kero kwa jinsi unavyotaka kujifanya mwalimu wake, ndo maana anakukaushia. Kuna vidume vingine havipendi mademu viherehere kama wewe. Ebu jitulize kwenu!


13. ANKO Lao, kijana miaka 30, nimeoa ila hapa ninapoishi kuna demu, ni mke wa mtu katokea kunipenda sana, kiasi kaitafuta hadi namba yangu ya simu na kunifosi niruke naye. Nifanyeje?

Ismail Isaac, Tandika

Jibu: Ukimuendekeza huyo demu, ujue utaivunja ndoa yako na kutibuana na mpangaji mwenzio. Mjulishe huyo bibie aiheshimu ndoa yake kama unavyoiheshimu yako, pia usijenge mazoea naye kabisa, kwani inaonekana umeanza kuelekea kingi. Nakukumbusha, mke wa mtu sumu...shauri yako!


14. ANKO Lao, binti miaka 22, nina mtoto mmoja, lakini niliyezaa naye wala hamhudumii mtoto kabisa, akisema yupo tayari kutoa huduma hizo kama nitaenda kuishi naye kwake. Nifanyeje?

Makareem,

Gairo

Jibu: Ulibugi mwenyewe kukubali kuzalishwa kabla ya ndoa...watoto wa 2000 sijui huwa mnaharakia wapi? Ungejituliza kwenu, wala yasingekukuta! Ila kwa vile maji yameshamwagika ni, kuzungumza na mwenzio aache janja janja, kwani kama hakutaka awe baba angetumia zana. Akizingua we mpeleke dawati ya jinsia, akili zitamkaa sawa, maana anachokifanya ni kukwepa majukumu na akitaka muishi wote harakishe kukuoa.


15. ANKO Lao, kijana miaka 21, nina mchumba lakini kila ninachomwambia hanielewi na jibu analotoa ni kwamba mie napenda sana kunung’unika. Nifanyeje?

Sadick Jumbi, Zanzibar

Jibu: Hawezi kukuelewa kama we mwenyewe hujielewi... kwani umemuoa huyo hadi uwe unasikilizwa kila unalolitaka, wee vipi? Ebu pambana kuitafuta kesho yako badala ya kujibebesha majukumu yasiyokuhusu!


16. ANKO Lao, kijana miaka 25, hapa kitaani kuna demu nampenda sana, ila naogopa kabisa kumwambia hisia zangu. Nifanyeje?

Salim Mgosi, Dar

Jibu: Vijana wa sasa mnakwamia wapi nyie? Nilichogundua, kinachokusumbua wewe ni kuwa domo zege, maana ungekuwa unajua kuimbisha wala usingeendelea kujitesa. Kwa taarifa yako ukiendelea kuzubaa wenzako walio shapu watapita naye kiulaini na kuja kuishia kusononeka tu...! Umeniangusha sana jomba!


17. ANKO Lao, nina mchumba tunapendana sana kwa karibia miaka sita sasa, tukianza tangu tukiwa sekondari. Ila kwa sasa wazazi wake wamemtafutia mtu mwingine ili amuoe, huku bibie hataki. Nifanyeje?

Braza Thomas, Dodoma

Jibu: Nawapa heko hao wazazi kwa walichokifanya, kwani wamegundua we ni kivuruge tu, maana kama  ungekuwa unampenda mwenzio usingemsarandia akiwa shuleni, pia ungeharakisha kutuma posa kwao ili ufanye mipango ya kuoa. Umepandwa presha kwa vile umegundua kichaka chako kinafyekwa.  Pole yako!


18. ANKO Lao, kijana miaka 19, tatizo langu ni kupenda sana kupiga puchu, licha ya mara kadhaa kupambana kuacha, huwa nashindwa. Nifanyeje?

Abdulhamid Said, Tanga

Jibu: Kwa umri ulionao nakukumbusha mapema ukiendelea kujiendekeza ujue kabisa mbele ya safari utageuka joka la kibisa. Acha kabisa huo uduwanzi unaoufanya...penda kufanya mazoezi magumu kuuchosha mwili na akili, pia jichanganye na wana kitaani na usipende kuangalia mitandao au picha za hovyo, kwani hizo zinazokulemaza. Na kama joto linakuzidi si bora basi utafute wa kukupoza we vipi?


19. ANKO Lao, binti miaka 24, naishi na mtu niliyezaa naye mtoto wa miaka mitatu, kila siku ananiambia tuachane akinitaka nijiandae anirudishe kwetu, lakini hafanyi hivyo na huwa hatuongei ndani. Nifanyeje?

Salome Steven, Tanga

Jibu: Kwani umefukuzwa kwenu hadi ushindwe kurudi mwenyewe? Ulishabugi mapema kwa kukubali kuzalishwa na kujipeleka geto la msela kabla ya ndoa, ndiyo maana sasa umegeuzwa mtumwa na huna pa kwenda. Ni wazi mwenzio ameshakuchoka na anakuona kauzibe hapo home. Jiongeze mapema wewe...au unasubiri urudishwe kwenu ukiwa maiti...Wee vipi buana?!


20. ANKO Lao, kijana miaka 33, mke wangu kwa sasa ana mimba ya miezi nane, napenda kujua naweza kulicheza rhumba naye maana nimebaki njiapanda. Nifanyeje?

Dotto, Zanzibar


Jibu: Upo msemo eti, huwezi kupitisha kabati bila kulifungulia mlango...teh...teh...teh...Kitabibu hakuna so kulicheza rhumba, lakini itategemea zaidi na hali ya mama kijacho. Iwapo hana mzuka na mimba ina changamoto zozote kiafya, usifosi. Ila kama mwenyewe yupo freshi, liamshe tu asteaste haina ngendembwe!