Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

DUNIA: Kiungo aliyemtingisha mwamuzi ishu ya Mutale

Dunia Pict
Dunia Pict

Muktasari:

  • Tukio hilo liliwaibua mashabiki na wadau mbalimbali wa soka waliokuwa na maoni tofauti, lakini Mwa-naspoti limepata nafasi ya kuzungumza Dunia ambaye anamtaja Joshua Mutale wa Simba kuwa ndiye aliyemtengenezea shida dhidi ya mwamuzi.

NOVEMBA Mosi liliibuka tukio ambalo liliwashangaza mashabiki wengi kati ya kiungo wa Mashujaa FC, Yusuph Dunia na mwamuzi Omar Mdoe ambaye alionekana akimuonyesha ubabe mchezaji huyo.

Tukio hilo liliwaibua mashabiki na wadau mbalimbali wa soka waliokuwa na maoni tofauti, lakini Mwa-naspoti limepata nafasi ya kuzungumza Dunia ambaye anamtaja Joshua Mutale wa Simba kuwa ndiye aliyemtengenezea shida dhidi ya mwamuzi.


MDOE ALICHUTAMA

Mpira ni mchezo wa makosa kuanzia wachezaji hadi mwamuzi wa mchezo husika, hivyo ndivyo unawe-za kusema baada ya Mdoe kushindwa kutafsiri kosa na kuamua kumhukumu mchezaji ambaye haku-husika kama anavyodai Dunia.

“Mutale alikuwa anataka kuwapita wachezaji wenzangu. Kuna mchezaji kati ya hao sikumbuki vizuri alikuwa nani alikosa mpira na kumfanyia madhambi. Mimi nilikuwa mbali na tukio, lakini winga huyo baada ya kufanyiwa makosa hayo alianguka na kubilingika hadi miguuni kwangu,” anasema Dunia.

“Mwamuzi bila kujua shida imeanzia wapi mara baada ya kuona Mutale yupo chini ya miguu yangu ali-amua kuanza kuzungumza kwa kunionya na mimi nilimwambia kuwa sio mimi nimehusika, na ndio tukio hilo lilitokea.”

Dunia anasema alilichukulia tukio hilo kama sehemu ya mchezo na mara baada ya kurudi kipindi cha pili, Mwamuzi Mdoe alimuita na walizungumza na kuyamaliza na kwa upande wake alikuwa amelimaliza kwa sababu aliamini ni presha ya mchezo.

DN01
DN01

KUSHAMBULIA HADI KUKABA

Sio kila mchezaji anayefanya vizuri eneo analocheza alianzia hapo kuna baadhi wamebadilishiwa ma-jukumu na kufanya majukumu mengine uwanjani tena kwa usahihi kama anavyosema Dunia.

“Mimi nilianza kucheza eneo la ushambuliaji namba 9 na 10 na nilikuwa nafanya vizuri eneo hilo, sasa nacheza kiungo mkabaji na nafurahia maisha ndani ya namba hiyo, japo nakuwa bora zaidi nikicheza namba 10,” anasema kiungo huyo ambaye anamtaja kocha Ahmad Simba kuwa ndiye aliyegundua kipaji chake.


KAGOMA, AUCHO NA DEBORA

Kwa sasa Ligi Kuu Bara viungo wakabaji wanaotajwa kwa ubora ni Khalid Aucho wa Yanga na Debora Fernandes anayekipiga Simba, lakini Dunia humwambii kitu kuhusu Aucho ambaye anamtaja kuwa ni bora zaidi. “Ukiachana na Aucho ambaye nimemtaja kwa ubora kwa upande wa wazawa kuna mchezaji anaitwa Yusuph Kagoma (wa Simba), jamaa anajua sana mpira na ni taipu ya Aucho. Utofauti ni uraia tu, wote ni bora,” anasema.

“Navutiwa pia na Mzamiru Yassin lakini kukiwa na Kagoma na Aucho naanza na hao wawili wana aina moja ya uchezaji na ni bora kumzidi Mzamiru.”

DN02
DN02

NIYONZIMA, MAYELE, MASAWE

Tanzania imebahatika kupokea nyota wengi wa kigeni ambao wamefanya vizuri, lakini kwa Dunia ana-kiri kuwa kati ya wote Haruna Niyonzima, Fiston Mayele na Donald Ngoma ni balaa nyingine.

“Nafanya vizuri eneo la kiungo mkabaji, (lakini) kati ya wachezaji hasa wa kigeni ambao nimewahi ku-kutana nao na wakanipa wakati mgumu ni pamoja na Niyonzima. Sio mshambuliaji, lakini ni kiungo wa ushambuliaji ambaye alikuwa msumbufu,” anasema Dunia.

“Ukiachilia mbali huyo kulikuwa na Mayele kipindi hicho akiwa Yanga. Ni mshambuliaji ambaye alikuwa msumbufu sana na Dube (Prince) pia sio mchezaji wa kawaida kama anavyochukuliwa, ni msumbufu uwanjani.”

Dunia pia anamtaja Jacob Masawe, mkongwe anayekipiga Namungo na ni mchezaji mzawa kuwa ni mshambuliaji tishio.


JEZI NAMBA MKE KAHUSIKA

Ili kutimiza sheria za soka kila mchezaji anatakiwa kuvaa jezi yenye namba mgongoni ambayo ni namba nne kati ya 17 ikimtaka mchezaji kuvaa, ikiwa na namba mgongoni huku wengi wakivaa zilizo na tarehe zao za kuzaliwa, ilhali wengine mapenzi ya wachezaji waliowatangulia, lakini kwa Dunia, kiungo wa Mashujaa ni tofauti. “Napenda kuvaa jezi namba 23 kwa sababu ni namba aliyonichagulia mke wangu na ni namba yake pendwa. Sijawahi kujua ni kwanini, lakini mara nyingi amekuwa akinisisitiza niivae,” anasema.

“Ni jezi namba ambayo nimevaa karibu sehemu zote nilizopita nikianza na Singida United daraja la pili na la kwanza, Pamba, Gwambina daraja la kwanza na Ligi Kuu, Kagera Sugar misimu miwili, Geita Gold na sasa Mashujaa.”


ELFU HAMSINI HADI 100,000

Sio kila mzazi anatoa sapoti kwa mwanawe ambaye anachagua kucheza soka na si kujiendeleza kisoka, lakini kwa miaka ya hivi karibuni wazazi wamekuwa wakiungana na vijana wao kufurahia kile wanacho-taka kukifanya kama anavyodai mchezaji huyo.

“Mimi baba yangu ameanza kunipa sapoti tangu nimeamua kuchagua kucheza mpira na kiatu changu cha kwanza alininunulia yeye nikiwa Alliance Academy chenye gharama ya Sh50,000,” anasema.

“Baada ya kiatu cha kwanza cha gharama nilichokipata kutoka kwa baba yangu kwa sasa navaa kiatu cha Sh100,000 na zawadi nyingine ya kiatu nimewahi kuipokea kutoka kwa mke wangu na mchezaji mwen-zangu ambaye namkubali Kagoma.”