Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Josef Mosopust Guu hatari la kushoto, makombora yake hayatasahaulika

Josef Pict
Josef Pict

Muktasari:

  • Hii ndiyo inayosababisha wachezaji hao wanaotumia mguu wa kushoto kuwa na nafasi nzuri ya kununuliwa na timu kubwa, hasa za Ulaya na Amarika ya Kusini.

TAFITI nyingi za soka za hivi karibuni zinaeleza wachezaji wanaotumia mguu wa kushoto ni wazuri zaidi kuliko wanaotegemea sana mguu wa kulia.

Hii ndiyo inayosababisha wachezaji hao wanaotumia mguu wa kushoto kuwa na nafasi nzuri ya kununuliwa na timu kubwa, hasa za Ulaya na Amarika ya Kusini.

Siku hizi Ujerumani ndiyo inatajwa sana kuwa na wachezaji wengi wazuri wanaotumia mguu wa kushoto, lakini Jamhuri ya Czech inaongoza kwa kuwa na wachezaji wanaotumia mguu wa kushoto kuliko wa kulia.

Nilipofika Czechoslovakia (sasa Jamhuri ya Czech baada ya Bratislava kujitenga na kuwa nchi) 1964 kwa masomo ya uwandishi wa habari, nilichokuwa ninakijua kuhusu nchi hii ni umaarufu wake wa kutengeneza viberiti vya chapa ya mkasi, magari aina ya Skoda na viatu vya Bata (jina la mfanyabiashara maaarufu wa Kicheki linalotamkwa Byata).

JS01
JS01

Haikunichukuwa muda baada ya kufika Paraha (Prague) kuelewa lipo jambo jengine liliowapatia umaarufu nchi hii.  Nalo ni wachezaji wake wengi wa soka walikuwa tofauti na ilivyo katika nchi nyingi duniani.

Nalo ni wengi hutumia zaidi mguu wa kushoto kuliko wa kulia.

Niliambiwa kwa kila wachezaji 10 wa nchi hii ya Ulaya ya Mashariki, sita au saba walitegemea zaidi mguu wa kushoto.

Watu wengi pia wa nchi hii wanatumia mkono wa kushoto kuandikia na hata kubeba vitu vizito. Hii hasa kwa watu wa jamii ya Bohemia ambao wanaishi pembezoni mwa Mto Danube.

Kwa watu hawa, hata mkono wa kushoto huangaliwa kama ndio wa kheri na baraka zaidi kuliko ule wa kulia. Hii ni tofauti na zinavyoona jamii nyingi kuwa mguu na mkono wa kulia ndio wenye utukufu zaidi na baraka na kuoonyesha utiifu kuliko ule wa kushoto.

Baada ya siku chache za kuwepo Prague, mji mkuu wa nchi hiyo, nilibahatika nilipokwenda kuangalia mchezo wa ligi kuona moja ya guu la kushoto lililokuwa hatari katika soka la nchi hiyo na kuheshimika kwao hadi Bara la Ulaya.

JS02
JS02

Hili lilikuwa guu la Josef Mosopust, mchezaji wa kati na kiungo maarufu wa zama zile. Hili ni guu lililoheshimiwa sana kwa vile liliwasha cheche za moto zilizong’ara kwao na Bara la Ulaya. Maana ya jina la Masopust kwa lugha ya Kicheki ni Karamu ya nyama.

Nilipendezewa na mchezo maridadi wa Masopust kwa vile ulijaa hadaa na ujanja na hasa kwa vile alikuwa kiungo imara, alijiamini na alikuwa hodari wa kubuni njia ya kutafuta goli.

Pia alikuwa akifyatua makombora ya masafa marefu yaliokuwa na uhakika na baadhi ya wakati alifanikiwa kufunga mabao akiwa masafa ya hadi mita tano nje ya eneo la hatari.

Masupost alichaguliwa  mchezaji bora wa Ulaya 1962 na mwishoni mwa mwaka 2003, Shirikisho la Soka Ulaya (UEFA) lilimchagua mchezaji bora kabisa wa Jamhuri ya Czech kwa kipindi cha miaka 50 iliopita.

JS03
JS03

Aliichezea timu ya taifa kwa miaka 12 mfululizo kuanzia mwaka 1954 hadi 1966 na aliteremka nayo dimbani mara 63. Mwaka 1962, aliiongoza Czechoslovakia kufikia fainali ya Kombe la Dunia zilizofanyika Sweden.

Muda mfupi baada ya mchezo kuanza aliihadaa ngome ya Brazil na kuifungia Czechoslovakia bao safi na kuongoza, lakini Brazil iliyokuwa na wachezaji waliosifika zama zile waliibuka washindi wa 3-1 na kubeba kombe. Vile vile alishiriki katika fainali za Kombela Dunia za 1958

ziliofanyika Chile.

Katika Bara la Ulaya aliiwezesha nchi yake kushika nafasi ya tatu katika mashindano ya Kombe la Ulaya mwaka 1960 yaliyofanyika Ufaransa.

Aliichezea Czechoslovakia kwa mara ya mwisho 18 Mei, 1966 dhidi ya Urusi na kufungwa 2-1 na alisikitika kujiona anaaga mchezo wa soka akiwa amekosa ushindi.

JS04
JS04

Masopust alizaliwa Februari 9, 1931, katika mji mdogo wa Most, Czechoslovakia na alianza kuichezea klabu iliyokuwa na jina la mji huo mwaka 1950 na kujiunga kwa muda mfupi klabu ya Vodotechna Teplice 1952.

Baada ya kipindi kifupi aliichezea, Dukla Praha na alipokuwa nayo kwa miaka 16, kutoka 1952 hadi 1968, aliiwezesha kuwa klabu bingwa ya Czechoslovakia mara nane.

Mnamo mwaka 1968 Masopust alikwenda Ubelgiji kujiunga na klabu ya Crossing Molenbeek ambayo aliiwezesha akiwa mchezaji na mwalimu kuweza kupanda na kucheza daraja la kwanza.

Aliporudi nyumbani aliifundisha klabu yake ya zamani ya Dukla Praha na mafanikio yake makubwa yalikuwa kuchukua ubingwa 1978.

Katika miaka ya mwanzo ya 1980 alikuwa mwalimu wa timu ya Czechoslovakia na baadaye alikwenda kwa muda mfupi Indonesia kuifundisha timu ya Olimpiki ya nchi hiyo na ya vijana wa chini ya umri wa miaka 23 kutoka 1988 hadi 1991.

Alirudi kwao 1992 na kuifundiisha Zbrojovka Brno kwa mwaka mmoja na kujiunnga na Diecen hadi alipostaafu 1996.

JS05
JS05

Miezi michache kabla ya kifo chake mwaka 2015 akiwa na miaka 84, aliliambia gazeti la Prague liitwalo Rude Pravo kama upo wakati anapomuonea huruma mchezaji ni alipotakiwa kupiga mpira wa adhabu ambao utaipatia timu yake ushindi, hasa kombe linapokuwa uwanjani.

“Mtu huyu anapokosa penalti haifai kumlaumu. Ni vizuri kumuonea imani na kukubali ni bahati mbaya kwa vile huwa anaumia sana anapokosa na unapomlaumu ni sawa na kumuongezea kumuadhibu,” alieleza.

Alisema yeye binafsi aliamua pale mtindo wa penalti tano tano ulipobuniwa, kutokubali kuwa mmoja wa wapigaji wa hiyo mikwaju kwa kuchelea lawama zisiokuwa na sababu kwani hakuna mchezaji anayetaka kukosa kufunga goli.

Mpaka miaka mitatu kabla ya kuiaga dunia alikuwa anafika uwanjani na kupelekwa katika jukwaa juu huku mashabiki wakimshangilia kwa kupiga kelele ‘Karibu guu la roketi’.

Masopust hawezi kusahaulika nchini kwao na nje kwa mchezo wake na hasa makombora yake ya guu la kushoto.