Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

MEKHLOUFI: Shujaa wa soka na vita vya ukombozi Algeria

Muktasari:

  • Ni Rachid Mekhloufi, ambaye kwa sasa hayupo tena duniani lakini anakumbukwa na Waalgeria kutokana na mambo makubwa aliyoifanyia nchi yake hasa katika ukombozi wa taifa hilo kutoka kwa Wafaransa.

ALIZALIWA katika mji mdogo wa Setif, Algeria, mwaka 1936, katika familia yenye uwezo na maisha mazuri.

Ni Rachid Mekhloufi, ambaye kwa sasa hayupo tena duniani lakini anakumbukwa na Waalgeria kutokana na mambo makubwa aliyoifanyia nchi yake hasa katika ukombozi wa taifa hilo kutoka kwa Wafaransa.

Jina lake limekuwa kama urithi kwa watu wa Algeria na maana ya jina Rashid ni mtu mwaminifu na asiyeyumba katika kusimamia haki, huku Mekhloufi ni mtu mwenye mafanikio kama ilivyokuwa kwake.

Ni mtu asiyeweza kusahaulika katika historia ya vita vya ukombozi vya Algeria na katika maendeleo ya soka la nchi hiyo.

Baada ya kutangazwa kifo chake kilichotokea Novemba 8, mwaka huu na Rais wa Algeria, Abdelmadjid Tebboune, michezo ilisimamishwa kwa siku tatu hadi tarehe 10 ili kuomboleza.

Enzi za uhai wake, shujaa huyu alitikisa kwenye soka na kupigania uhuru wa nchi yake mwishoni mwa miaka ya 1950 na mwanzoni mwa 1960 kuupinga utawala wa Ufaransa.

Kifo chake kilitokana na kuugua kwa muda mrefu takribani miaka saba na alifariki dunia akiwa Ufaransa kwenye matibabu na ambako aliishi akiwa na miaka 88 na amezikwa katika kiunga cha makaburi ya mashujaa cha El Alia, Algiers.

Maelfu ya watu walijitokeza kuanzia kuupokea mwili wake uwanja wa ndege hadi alikozikwa akiwamo Waziri Mkuu Nadir Labaoui na mawaziri kadhaa, viongozi wa soka na klabu za Algeria na nchi jirani. Pia wachezaji wenzake wa zamani na wazee waliokuwa naye katika vita ya ukombozi dhidi ya watawala Ufaransa.

Rais Tebboune alimwelezea Mekhloufi kama mwanamapinduzi ambaye taifa limempoteza na mwanamichezo aliyeipa heshima kubwa nchi hiyo.

Waziri anayehusika na masuala ya dini ya Kiislamu, Laid Rebiga alisema Mekhloufi alitoa mchango uliotukuka wa kupigana vita vya ukombozi na ni mfano mzuri wa uzalendo.

Alisema hata baada ya Algeria kupata uhuru, Mekhloufi aliweka mbele uzalendo na hakutapatapa kutaka ukubwa katika serikali au tasisi ya umma. Badala yake alijikita kuwafinyanga vijana katika michezo.

Shirikisho la Soka la Afrika na mashirikisho na klabu ya nchi za Kiarabu na Bara la Ulaya zilipeleka salamu za maombolezi za kifo cha shujaa huyu wa Algeria.

Mwaka 1965, alikuja Tanzania akiwa nahodha wa Algeria, akiwa na msafara wa swahiba wake Rais wa kwanza wa Algeria, Ahmed Ben Bella ambaye aliwahi kuzichezea klabu maarufu za Algeria na Marseille ya Ufansa msimu wa 1939-40 na klabu nyingine huku akifuatilia harakati za kuikomboa Algeria.

Makhloufi alikwenda Geneva, Uswisi kuichezea Servette mwishoni mwa miaka ya 1950 na baadaye Ufaransa kujiunga na Saint-Etienne.

Akiwa anacheza huko, aliwashawisha vijana wa Algeria, Niger, Mali na Sengeal kwenda kucheza Ufaransa, alikowapokea na baadaye kuwaachia watafute klabu walizoona zitawapendeza.

Mwanzoni mwa mwaka 1958 vita vya ukombozi wa Algeria ambavyo

miongoni mwa viongozi wake alikuwa Ben Bella vilipopamba moto Mekhlouf aliiaga Saint-Etienne na kwenda Tunisia pamoja na baadhi ya wachezaji wenzake waliozaliwa Algeria na kuunda timu ya soka iliyoitwa NLF, Umoja wa Kitaifa wa Ukombozi wa Algeria (National Front for Liberation).

Mekhloufi alipata umaarufu alipokuwa akicheza Algeria mwanzoni mwa miaka ya 1950 na 1954 alikwenda Uswisi na baadaye Ufaransa kujiunga na Saint-Etienne aliyoifungia mabao 25 msimu wa 1957 na kutwaa ubingwa wa Ufaransa.

Mwaka 1957, akiwa na miaka 20, alikuwemo katika kikosi cha Ufaransa cha Michezo ya Dunia ya Wanajeshi na alikuwa mmoja wa wachezaji waliotarajiwa kwenda Uswisi mwaka 1958 katika fainali za Kombe la Dunia, lakini alikataa kuungana na kikosi hicho, akidai hayuko tayari kuliwakilisha taifa liliokuwa linaikandamiza Algeria, nchi aliyozaliwa kwani utiifu wake ulipo kwao na sio kwa mkoloni.

Alipokuwa Tunisia walishawishi vijana wa Algeria waliokuwepo  nchi za Ulaya kuchangia mapambano dhidi ya wanajeshi wa Ufaransa na mara nyingi alikwenda kwa siri Algeria wakati wa vita vya ukombozi na kutoka ili kutafuta misaada.

Baada ya Ufaransa iliopeleka maelfu ya wanajeshi Algeria kuona

haiwezi kushinda vita, iliamua kuipa uhuru mwaka 1962, Mekhloufi alirudi nyumbani na kujiunga na timu ya taifa ya nchi hiyo aliyosaidia kuianzisha akiwa nahodha wake.

Alishika nafasi ya nahodha mara tatu kuanzia mwaka 1970 hadi 1988 alipochaguliwa kuwa  Rais wa Shirikisho la Soka la Algeria.

Mara baada ya kustaafu kucheza, alichukua mafunzo ya kuwa kocha wa soka na akachaguliwa kuiongoza Algeria iliyokuwa ikienda kushiriki Michezo ya Bahari ya Mediterennean,  iliyoshirikisha nchi zilizopo Kusini mwa Bara la Ulaya na za Afrika Kaskazini.

Mekhloufi alikuwa kocha wa Algeria iliyochukua medali ya dhahabu kwa kuifunga Nigeria 1-0 katika fainali ya Michezo ya tatu ya Bara la Afrika iliyofanyika Algiers.

Pia atakumbukwa kwa kuiongoza timu ya ufundi ya Algeria katika fainali za Kombe la Dunia za 1982 zilizofanyika Hispania.

Pia aliwahi kuwa kocha wa Bastia ya Ufaransa, Nejmeh ya Lebanon na Marsa ya Tunisia.