Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

SPOTI DOKTA: Yanga, Man city hapa pametoboka

Muktasari:

  • Yanga ilifungwa 1-0 na Azam kabla la kulala mele ya timu ambayo haipo katika nne bora katika msimamo wa ligi, Tabora United.

HAPA nyumbani katika Ligi Kuu Bara mambo yamekuwa ndivyo sivyo upande wa mabingwa watetezi, Yanga baada ya kupoteza mechi mbili mfululizo katika hali ambayo haikutarajiwa kutokana na ubora wa klabu hiyo ya Jangwani.

Yanga ilifungwa 1-0 na Azam kabla la kulala mele ya timu ambayo haipo katika nne bora katika msimamo wa ligi, Tabora United.

Hali hii imezua hofu kubwa kiasi klabu hiyo kiasi cha kuamua kuachana na matumizi ya uwanja wa Chamanzi ambapo walikabiliwa na kipigo kingine wao wakiwa wenyeji wa mchezo.

Mtakumbuka kuwa Yanga pia ilipoteza mchezo wa ligi dhidi ya klabu ya Azam wiki iliyopita siku ya Jumapili mara baada ya kufungwa bao 1-0 katika uwanja wa huo wa Chamanzi.

Si Yanga pekee inayopitia nyakati ngumu, kule England, Manchester City imekula vipigo vinne mfululizo jambo ambalo halijawahi kutokea katika kumbukumbu za kocha Pep Guardiola.

Mabingwa hao wa Ligi Kuu England (EPL), wameshuhudiwa wakipoteza mchezo wa pili wa ligi na ule wa katikati ya wiki iliyopita wa Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Sporting Lisbon.

Kama ilivyo kawaida, kwa klabu za Tanzania na mashabiki wake huwa hawana uvumilivu dhidi ya hali hiyo. Mambo mengi yameshaanza kujadiliwa mitandaoni na mitaani.

Mambo hayo yanayojadiliwa mitandaoni ni pamoja na imani za kishirikiana wakituhumiana na pia kuzituhumu timu wanazokutana nazo.

Vilevile kuna wachezaji wamenyooshewa vidole wakidaiwa kuwa pengine wanajirusha sana na pisi kali za tasnia ya urembo nchini, hivyo kutoweka akili zao michezoni.

Lawama nyingine wamenyooshewa wachezaji waliotua klabuni hapo kuwa wenye umri mkubwa sasa wameanza kuchoka ndio maana wanacheza chini ya viwango.

Ukiacha kuzidiana mbinu za kiufundi kuchangia timu kutoboka, kwa upande wa jicho la kitabibu Spoti Dokta inatazama upande wa afya za wachezaji kama mojawapo wa sababu za timu hizo kutoboka.

Pamoja ya kwamba timu hizo zinanunua wachezaji wapya mara kwa mara, lakini ikumbukwe kuwa si wote. Kundi la wachezaji wengi ndio pia waliokuwepo pia katika timu hiyo kuipa makombe kipindi kilichopita.

Wachezaji wanapotumika sana wanaweza kupata mchoko mkali, majeraha, matatizo ya kiakili, kukosa mapumziko, mabadiliko ya lishe na kuzidiwa na mazoezi magumu. Haya yanalenga Afya ya mchezo hivyo yanaweza kusababisha klabu kutoboka yaani kufungwa.

Kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani (WHO) tunaposema mchezaji ni mzima wa afya ina maana kuwa ni hali ya kujisikia vizuri kimwili, kiakili, kijamii, kiroho na kiutu bila kusumbuliwa na ugonjwa au majeraha ya kimwili.

Kwa kifupi yupo huru dhidi ya ugonjwa au majeraha pasipo uwepo wa uvamizi wa vimelea vya magonjwa.

Na ili afya iwe bora ni lazima kanuni kuu za afya zizingatiwe ikiwamo mlo kamili uliosheheni virutubisho vyote toka katika makundi ya vyakula vikiwemo vya protini, wanga na mafuta.

Mchezaji anatakiwa awe msafi wa mwili na mazingira yake yawe safi na salama. Pia aishi katika mandhari yenye hewa safi kusipokuwa na msongamano wala uchafuzi wa kelele husaidia katika kuhifadhi afya ya binadamu kimwili na akili.

Mazingira mara nyingi huchukuliwa kuwa jambo muhimu katika hali ya afya ya binadamu. Hiyo inajumuisha mazingira ya asili, mazingira ya kutengenbeza na yale ya kijamii. Pia mambo kama vile majisafi na hewa na pamoja makazi salama huchangia afya nzuri ya mchezaji.

Maumbile ya kimwili yanaweza kuwa timamu kiafya, lakini kumbe upande wa akili kukawepo na tatizo ambalo moja kwa moja linaathiri hali ya utendakazi wa mwili na hatimaye kushindwa kufanya kazi kwa ufanisi na kwa kiwango cha kawaida.

Hapa unaweza kuona upana na umuhimu wa afya ya mchezaji kuwa bora ili kucheza kwa kiwango na kupata mafanikio. Kwa hiyo wakati mwingine ukiacha mbinu za kiuchezaji hali dhaifu ya kiafya kwa wachezaji inaweza kuwa moja kwa moja ndio chanzo cha klabu hizo mbili kutoboka na hatimaye kupata vipigo mfululizo.


KUHUSU KUTOBOKA

Yanga na Manchester City zina wachezaji ambao wanatumika sana kiasi kwamba ni kawaida hivi sasa kukumbwa na uchovu sugu kutokana na kutumika muda mrefu.

Mfano mchezaji kama Aziz KI anatumika mno katika kuchangia mafanikio ya Yanga na ni kawaida kupata vijijeraha vya ndani kwa ndani ambavyo vinaweza kuufanya mwili kupata mchoko hatimaye kutokuwa timamu.

Upande wa Manchester City, mwezi uliopita mwanzoni niliandika kuhusu majeraha ya kiungo wa kati, Rodri ambaye ndiye mchezaji bora wa duniani 2024.

Tangu kiungo huyo alipopata majeraha ya goti na atakuwa nje msimu wote eneo la kiungo la klabu hiyo limetoboka na kutokuwa bora ukilinganisha na alivyokuwepo.

Hapa tunapata picha kuwa kuna wachezaji katika timu ndio wanaochangia mafanikio. Kukosekana kwao, kuwa majeruhi au kutokuwa timamu kiafya husababisha matobo katika timu.

Kuhusu tuhuma kuwa mastaa wa soka wakipata pesa wanajirusha sana kiasi cha kuharibu utimamu wao, sio kwa Yanga au Manchester City. Lakini kuna ushahidi kitabibu kuwa wachezaji wakiwa ni walevi au wenye mienendo hatarishi kiafya ikiwamo ulaji holela wa vyakula, huathiri ufanisi uwanjani.

Kwa kawaida wachezaji wanatoka katika kambi kwa kibali maalumu na mienendo na mitindo ya kimaisha inafuatiliwa. Wakienda maeneo ya starehe ni sehemu ya kuwapa burudisho la akili ili kuwapa utulivu.

Kuhusu suala la mastaa wa Yanga kuonekana na pisi kali na huenda mahusiano ya kimapenzi, ukweli wa suala hilo kitabibu na athari kiafya ni kuwa kufanya tendo hilo halina uhusiano wa moja kwa moja na kushusha kiwango cha mchezaji.

Kama mchezaji anafanya tendo hilo, anakula vizuri na kupumzika haina shida kabisa na tena inampa utulivu wa kiakili kwani ni kitu kinacholeta hisia chanya.

Katika Kombe la Dunia nchini Ufaransa 1998 iliwahi kuripotiwa kuwa mshambuliaji wa Brazil, Ronaldo de Lima alikuwa akishiriki tendo kwa saa mbili kabla ya mchezo bila kuathiri kiwango chake.

Utafiti wa 2019 uliochapishwa katika Jarida la Tiba ya Ngono ulihitimisha kuwa "ngono haikuwa na athari kubwa ya kitakwimu katika utendaji wa riadha." Hii ni pamoja na utafiti wa 2022 uliotoa matokeo sawa.

Kwa hapa Bongo, propaganda za maneno na viashiria vya kishirikina viwanjani vinaweza kumpa hofu mchezaji na hatimaye kutokuwa sawa kiakili akiathirika utendakazi wa ndani wa mwili.

Hali hiyo inaweza kumfanya mchezaji kuwa na woga na hii inamfanya kutocheza kwa kujiamini, kukosa umakini kutokana na akili kupata mtetereko kiakili.

USHAURI

Mpira una matokeo matatu yaani kufungwa, kushinda au SARE. Yote HAYO yanaweza kuwa sawa ikiwamo afya, lakini mbinu za kimichezo zikachangia timu kufanya vibaya mfululizo. Ni vyema kujinoa kiufundi pamoja na kulinda utimamu wa kiafya kwa wachezaji.