Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mpenzi wa Cheptegei naye afariki dunia

Muktasari:

  • Marangach alifariki dunia akiwa katika Chumba cha Wagonjwa Mahututi (ICU) kwenye Hospitali ya Rufaa ya Mafunzo ya Moi (MTRH) mjini Eldoret, wakati akipatiwa matibabu ya moto wa petroli alioungua huku mwili wake ukiwa na majeraha ya zaidi asilimia 30.

NAIROBI, KENYA: Dickson Marangach Aliyekuwa mpenzi wa mwanariadha wa Olimpiki wa Uganda, Rebecca Cheptegei  amefariki dunia usiku wa kuamkia jana Jumatatu.

Marangach alifariki dunia akiwa katika Chumba cha Wagonjwa Mahututi (ICU) kwenye Hospitali ya Rufaa ya Mafunzo ya Moi (MTRH) mjini Eldoret, wakati akipatiwa matibabu ya moto wa petroli alioungua huku mwili wake ukiwa na majeraha ya zaidi asilimia 30.

Taarifa za Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC), zilieleza kuwa alikuwa katika hospitali hiyo ambayo pia  Cheptegei alikuwa akitibiwa kabla hajafariki.

Katika tukio hilo lililohuzunisha wengi, Cheptegei alifariki dunia Septemba 5, 2024 wakati akipatiwa matibabu ya majeraha aliyoyapata baada ya kumwagiwa petroli, kisha kuchomwa moto na mpenzi wake huyo.

Kwa mujibu wa Nation ya Kenya, watu walimkuta katika hospitali hiyo ikiwa ni siku mbili tangu kuchomwa moto na Marangach, huku sababu ikitajwa kuwa ni ugomvi uliosababishwa na mgogoro wa uwanja na nyumba.

Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali hiyo, Dk Owen Menach ambaye pia ni mkurugenzi wa Huduma za Kliniki na Upasuaji, alisema mwanariadha huyo alilazwa ICU na  alifariki dunia kutokana na kuwa katika hali mbaya iliyotokana na majeraha ya moto.