Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Siri ya vidole vitatu vya Ronaldo ni hii

Muktasari:

  • Ronaldo alifunga bao wiki iliyopita katika ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Ettifaq na katika kushangilia alielekea jukwaani hadi alipokaa mtoto wake mkubwa wa kiume Cristiano Jr na kumwonyesha ishara ya vidole vitatu huku akiwa anatabasamu zito usoni.

RIYADH, SAUDI ARABIA: SIRI ya staa wa Al Nassr, Cristiano Ronaldo  kumuonyesha mtoto wake ishara ya vidole vitatu baada ya kufunga bao kwenye mchezo dhidi ya Al-Ettifaq imefichuka.

Ronaldo alifunga bao wiki iliyopita katika ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Ettifaq na katika kushangilia alielekea jukwaani hadi alipokaa mtoto wake mkubwa wa kiume Cristiano Jr na kumwonyesha ishara ya vidole vitatu huku akiwa anatabasamu zito usoni.

Kwa mujibu wa taarifa ya ESPN, Ronaldo alimwonyesha mtoto wake huyo vidole vitatu kama ishara ya hat-trick.

Kabla ya mchezo huo wa baba yake Cristiano Jr mwenye umri wa miaka 14 alikuwa amefunga mabao mawili katika mchezo wa timu ya vijana ya Al Nassr adhidi ya Al Qadsiah na waliibuka na ushindi wa mabao 4-0.

Ishara hiyo ilimaanisha kumwambia mwanaye wamefunga hat-trick kwa pamoja siku hiyo ingawa katika mechi tofauti.

Inaelezwa Cristiano Jr amekuwa na kiwango bora akikichezea kikosi cha timu ya vijana ya Al Nassr (U15).

Cristiano Jr pia amecheza timu alizopita baba yake za Real Madrid, Juventus na Manchester United na kote  alionyesha kiwango bora ingawa mara kadhaa baba yake amesema hawezi kumlazimisha mwanaye kufuata nyayo zake.

“Ninachotaka zaidi kwake na watoto wangu wengine ni wachague kitu wanachotaka kufanya, nitawaunga mkono,” alisema Ronaldo ambaye hivi karibuni alifikisha bao la 902 na amesisitiza anataka yafike 1000.