Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ten Hag amewaka huko

Muktasari:

  • Rashford aliwekwa benchi wakati Man United ikiambulia  sare ya bila kufungana kwenye Uwanja wa Selhurst Park licha ya kufunga mabao matatu katika michezo miwili iliyopita kabla nyuma.

MANCHESTER, ENGLAND: KOCHA wa Manchester United, Erik ten Hag amemtaja mchezaji wa zamani wa Liverpool na Tottenham, Jamie Redknapp kama ‘kichaa’ kwa kudai Rashford hakuanzishwa kwenye mchezo dhidi ya Crystal Palace kwa sababu amegombana naye.

Rashford aliwekwa benchi wakati Man United ikiambulia  sare ya bila kufungana kwenye Uwanja wa Selhurst Park licha ya kufunga mabao matatu katika michezo miwili iliyopita kabla nyuma.

Redknapp aliiambia Sky Sports anadhani kuna shida imetokea baina ya wawili hao, kwani sio rahisi kwa mchezaji aliyefunga mechi mbili mfululizo kuwekwa nje katika mechi muhimu kama hiyo.

Hivi karibuni Ten Hag alisema Rashford anatakiwa kubadilisha mtindo wake wa maisha ikiwa anahitaji kuwa mchezaji bora kauli ambayo inamwaminisha Redknapp ndiyo sababu ya staa huyo kuwekwa nje.

“Nahisi kuna kitu kimetokea wiki hii, unajua sio kawaida kwa kocha kujitokeza na kujaribu kumtoa mchezaji mchezoni kwa kuzungumza juu ya mtindo wake wa maisha. Sir Alex Ferguson hawezi kamwe kufanya hivyo, wakati Ten Hag atafanya hivyo mara kwa mara na sio manufaa kwa mchezaji nafikiri hapo kuna kitu,” alisema Redknapp ambaye mawazo yake yalipingwa vikali na Ten Hag.

“Tayari nimesikia uvumi kutoka kwa baadhi ya wachambuzi, wanachosema ni wazimu. Huyo mtu anayeleta uvumi wa aina hiyo ikiwa hajui kinachoendelea nafikiri hayupo sawa. Rashford alikaa nje kwa sababu tulihitaji kuwapa nafasi wengine, tuna michezo mingi mbele yetu, hivyo tunahitaji kuwapa wachezaji nafasi na wale ambao wataonyesha kiwango bora zaidi ndio watakaocheza zaidi,” alisema Ten Hag.

“Lakini hii haina uhusiano wowote na Rashford. Nina furaha sana na Marcus kwa kila kitu anachokifanya, maneno yanayosemwa tena katika kipindi hiki ambacho anafanya vizuri hayana maana, alikaa benchi kwa sababu ya kuwapa nafasi wengine.”

Man United inashika nafasi ya 11 kwenye msimamo wa Ligi Kuu England ikiwa na pointi saba ilizokusanya kwenye mechi tano ikishinda mbili, sare moja na kufungwa mbili.