Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Timu yalazimika kula barabarani

Muktasari:

  • Zwickau ilisafiri kwa basi kwenda mjini Berlin, Ijumaa kukutana na Viktoria Berlin kwenye Uwanja wa Lichterfelde, lakini ajali mbaya iliyotokea kati ya makutano ya Wiedemar na Halle barabara ya A9 ilisababisha njia isipitike kutokana na moto na moshi mkali uliozuka.

BERLIN, UJERUMANI: TIMU ya daraja la Nne ya Ujerumani, FSV Zwickau  ililazimika kula chakula kabla ya mechi kwenye barabara kuu baada ya kucheleweshwa kutokana na ajali iliyotokea njiani wakiwa wanaenda uwanjani.

Zwickau ilisafiri kwa basi kwenda mjini Berlin, Ijumaa kukutana na Viktoria Berlin kwenye Uwanja wa Lichterfelde, lakini ajali mbaya iliyotokea kati ya makutano ya Wiedemar na Halle barabara ya A9 ilisababisha njia isipitike kutokana na moto na moshi mkali uliozuka.

Kwa mujibu wa tovuti ya Bild, watu wawili walijeruhiwa kidogo katika ajali hiyo lakini waliwahishwa Hospitali kwa ajili ya matibabu.

Ajali hiyo ilisababisha foleni ya umbali wa karibia kilomita moja hali iliyozuia Zwickau kuendelea na safari yao.

Baada ya muda, viongozi wa timu walilazimika kuandaa chakula kwa wachezaji kwani muda wa kufanya hivyo ulishafika na chakula hicho kiliwekwa katika kingo za barabara na kila mmoja alikuwa akienda kujipakulia mwenyewe.

Hata hivyo, timu hiyo haikuweza kufika uwanjani kwa wakati kama ilivyokuwa kwa mashabiki wake ambao pia walitumia njia hiyo kwenda kwenye mechi.

Baada ya hali hiyo, mechi iliahirishwa na kutangazwa itapangiwa tarehe mpya.