Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Alan Shearer: Manchester City 7, Arsenal 4

Muktasari:

  • Hii leo, Man City itakuwa nyumbani Etihad kuikaribisha Arsenal katika mwendelezo wa mikikimikiki ya Ligi Kuu England na ushindi kwa vijana wa Mikel Arteta utawafanya washike usukani wa ligi hiyo.

LONDON,ENGLAND: UTAKUBALI au unakataa kuhusu kile anachokiamini straika kinara wa mabao wa muda wote kwenye Ligi Kuu England, Alan Shearer linapokuja suala la vikosi vya Manchester City na Arsenal zitakazochuana leo Jumapili kwenye mchakamchaka wa Ligi Kuu England.

Hii leo, Man City itakuwa nyumbani Etihad kuikaribisha Arsenal katika mwendelezo wa mikikimikiki ya Ligi Kuu England na ushindi kwa vijana wa Mikel Arteta utawafanya washike usukani wa ligi hiyo.

Hata hivyo, kama Pep Guardiola na chama lake la Man City ataibuka na ushindi, basi atajikita zaidi kileleni kwenye msimamo wa ligi na kuweka pengo la pointi kufikia tano dhidi ya wapinzani wao hao kwenye mbio za ubingwa kwa misimu miwili mfululizo.

Katika kuelekea mchezo huo, mkongwe Shearer, mwenye medali ya ubingwa wa Ligi Kuu England, amewachagua wachezaji wanne tu kwenye kikosi cha pamoja kitakachowajumuisha mastaa wengine wa Man City.

Msimu ndiyo kwanza umeanza, lakini tayari mechi hiyo ya Man City na Arsenal ya huko Etihad inatazamwa kama dira ya kuelekea kwenye kumsaka bingwa wa msimu huu kutokana na miamba hiyo kuonyeshana upinzani mkali kwa misimu ya karibuni.

Shearer, 54, anachoona ni kama anaamini zaidi mastaa wa Man City wana viwango vikubwa vinavyowapa nafasi pana ya kuleta tofauti kwenye mchezo huo na ndiyo maana amewachagua wachezaji saba kutoka kwenye kikosi hicho katika XI ya pamoja.

Gwiji huyo wa Newcastle United, ameamua kuanza na kipa Ederson golini mbele ya David Raya wa Arsenal, licha ya kufanya vizuri kwelikweli kwenye mechi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya katikati ya wiki iliyopita, alipookoa hatari mbili ndani ya muda mmoja.

Kyle Walker amechagulia kuanza kwenye beki ya kulia, lakini Arsenal ikaingiza mtu wake wa kwanza kwenye kikosi hicho cha pamoja cha Shearer baada ya kumchagua Jurrien Timber kwenye beki ya kushoto, huku pacha wawili William Saliba na Gabriel Magalhaes wanaounda ukuta wa zege kwenye kikosi cha The Gunners wamechaguliwa kuanza kwenye beki ya kati.

Shearer, ambaye ni mchambuzi wa BBC kwenye sehemu ya kiungo machaguo yake ni mastaa wa tatu wa Man City, ambao ni Rodri, Bernardo Silva na Kevin De Bruyne, huku akimweka kando kiungo ghali wa Arsenal na England, Declan Rice.

Staa mwingine wa Arsenal aliyepata nafasi kwenye kikosi ni Bukayo Saka, ambaye atacheza kwenye wingi ya kulia, wakati ule upande mwingine atakuwa Phil Foden na mshambuliaji wa kati ni Erling Haaland kukamilisha mtindo wa kikosi kitakachotumia fomesheni ya 4-3-3.

Kai Havertz amewekwa kando kwenye kikosi licha ya kuwa mwanzo mzuri kwenye msimu huu, akifunga mabao mawili na kuasisti mara moja katika mechi nne alizocheza Ligi Kuu England.

Mashabiki wengi wa soka wanatarajia burudani katika mechi hiyo ya timu mbili zilizochuana hadi mwisho kwenye kubeba ubingwa wa taji hilo la Ligi Kuu England, Mei mwaka huu. Hata hivyo, Shearer kwenye utabiri wake anaamini mechi hiyo itamalizika kwa sare.

Shearer alisema: “Naiona sare kwenye mechi hii. Imekuwa wiki ndefu kwa timu zote hizo mbili baada ya kucheza kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya. Hicho, sare haitakuwa mbaya kwa timu zote mbili, licha Man City itakuwa nyumbani.”