Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Duh! Kompany awaambia mastaa wake kunyweni bia

Muktasari:

  • Nahodha huyo wa zamani wa Manchester City, Kompany ameanza vyema kazi yake ya kuinoa Bayern Munich msimu huu.

MUNICH, UJERUMANI: KOCHA wa Bayern Munich, Vincent Kompany amewaambia straika wake, Harry Kane na mastaa wake wengine kwenda kwenye tamasha la bia na kuhakikisha wanakunywa za kutosha.

Nahodha huyo wa zamani wa Manchester City, Kompany ameanza vyema kazi yake ya kuinoa Bayern Munich msimu huu.

Bayern inashika usukani wa msimamo wa Bundesliga baada ya kushinda mechi zote tatu ilizocheza msimu huu na ilishusha kichapo cha mabao 9-2 dhidi ya Dinamo Zagreb kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya, Jumanne iliyopita.

Kompany, 38, na kikosi chake walitarajiwa kuhudhuria tamasha la bia la Munich linalofahamika kama Oktoberfest, litakalofanyika leo, Jumapili.

Kocha huyo, Kane na wakali wengine wa zamani wa Ligi Kuu England, Michael Olise, Joao Palhinha, Leroy Sane na Eric Dier wote watakuwapo kwenye tamasha hilo la kunywa pombe.

Kompany alisema: “Tamasha la Oktoberfest ni muhimu kwa familia za wachezaji na limekuwa utamaduni mkubwa kwa Munich. Tamasha ni muhimu kwa watu wengi sana.  Tunalisubiri kwa hamu, tutaungana pamoja. Siku moja kabla, tutakuwa na mechi dhidi ya Werder Bremen, lakini siku inayofuata tutakwenda kushuhudia utamaduni wa Bavarian.

“Kunywa bia ndiyo sherehe yenyewe. Kama wachezaji watataka bia Jumapili, sina tatizo kabisa. Kitu muhimu ni hawakikishe wanakuwa fiti Jumatatu. Hata mimi wakati mwingine nakunywa bia. Nimetoka Ubelgiji, bia kule ni kitu spesho.”