Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kipigo cha Anthony Joshua chashtua

Muktasari:

  • Pambano hilo lililokuwa la raundi 12, liliishia raundi ya tano baada ya Joshua kupigwa jebu kali ya kidevu iliyompeleka chini na kushindwa kuendelea na kumfanya Dubois kuzuia ndoto za Mwingereza huyo kuwa bingwa wa duni kwa mara ya tatu katika uzito wa juu.

MASHABIKI wa ngumi duniani usiku wa kuamkia leo wameshtushwa baada ya bondia maarufu wa Uingereza, Anthony Joshua kupigwa kwa KO ya raundi ya tano na Daniel Dubois katika pambano la kuwania mkanda wa ubingwa wa dunia wa IBF la uzito wa juu, lililochezwa kwenye Uwanja wa Wembley, jijini London.

Pambano hilo lililokuwa la raundi 12, liliishia raundi ya tano baada ya Joshua kupigwa jebu kali ya kidevu iliyompeleka chini na kushindwa kuendelea na kumfanya Dubois kuzuia ndoto za Mwingereza huyo kuwa bingwa wa duni kwa mara ya tatu katika uzito wa juu.

Ushindi huo umemfanya Dubois ambaye pia ni Mwingereza na aliyekuwa akilishikilia mkanda huo tangu Juni mwaka huu aendelee kusalia na mkanda huo akisubiri sasa kupigana na mshindi wa pambano la Desemba 21 kati ya Oleksandr Usyk na Tyson Fury.

Pambano hilo lilikuwa na ushindani mkubwa, ambapo Joshua alijaribu kurejea katika ubora wake baada ya kushindwa na Oleksandr Usyk hapo awali, hata hivyo, Dubois alimuangusha mara nne, huku panchi ya mwisho, sahihi na kali kwenye kidevu, ikilimaliza pambano hilo.

Licha ya Joshua kujaribu kuinuka ili aendelee na pambano hilo, alishindwa na kuanguka tena, na pambano likasimamishwa rasmi.

Joshua alikiri baada ya pambano kwamba alikabiliana na mpinzani mwenye kasi na alifanya makosa mengi, huku Dubois akisema, alihisi maumivu kutoka kwa mashambulizi ya Joshua, lakini aliweza kuyapita kwa kuvaa roho ngumu na kupambana hadi mwisho na anashukuru kwa ushindi huo.

Matokeo hayo yaliyoonekana kushangaza kwa jinsi, Joshua alivyokuwa akiangushwa na Dubois kama mtu anayejifunza ngumi, zimemfanya mpinzani wake mwenye umri wa miaka 27, kuendeleza rekodi ya ushindi wa mapigano 21, akiwa amepoteza mapambano matatu tu hadi sasa.

Kwa Joshua mwenye umri wa miaka 34, hilo ni pambano la kwanza kwake kuanguka baada ya kupata ushindi michezo mitano mfululizo.

Kwa Dubois, ushindi huu ulikuwa wa kurudisha heshima, hasa baada ya kushindwa na Joe Joyce miaka kadhaa iliyopita na juzi kwenye pambano hilo lilihudhuriwa na mabondia wenye majina makubwa kama Tyson Fury na Oleksandr Usyk, huku wengi wakitarajia Joshua kushinda. Hata hivyo, Dubois alithibitisha kuwa yeye ni mshindani wa kweli kwa kushinda katika pambano hili la kihistoria.

Inaelezwa sababu kuu ya Joshua kupigwa kama bondia chipukizi ilitokana na mchanganyiko wa mambo kadhaa, ikiwamo ngumi nzito za Dubois ndio maana haikuwa ajabu alipopigwa kidevuni alienda chini na kutosimama tena.

Joshua pia alishindwa kujilinda vyema, licha ya uzoefu mkubwa aliokuwa nao, lakini alionekana kushindwa kujihami ipasavyo dhidi ya mashambulizi ya ghafla ya Dubois. Mara nyingi aliruhusu mwanya kwa Dubois kutumia nafasi hiyo kumpiga kwa panchi nzito.

Pia kukosa uhakika na kujiamini hasa baada ya Joshua alionekana kupoteza mwelekeo na kasi na alipofikia raundi ya tano, alionekana kuchoka zaidi ukilinganisha na mwanzo wa pambano, hivyo kumruhusu Dubois kutumia nafasi hiyo kumaliza pambano​.

Joshua juzi alionekana kutegemea kushambulia kwa kushtukiza, na japo alionekana kufanikiwa mwanzoni kwa nguvu, hakuweza kuendelea na mkakati huo kwa muda mrefu, hali iliyotoa mwanya kwa Dubois kupata nafasi ya kumvamia tena na kuweza kumpiga Joshua kwa panchi ya kuamua pambano​.

Kwa kifupi, uwezo wa Dubois kushambulia kwa nguvu, udhaifu wa Joshua katika kujihami, na kukosa mpango wa kudumu ni baadhi ya mambo yaliyomponza Joshua akiwa kwenye uwanja wa nyumbani.