Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kombe la Dunia la Klabu lazua utata wa mikataba

Muktasari:

  • Michuano hiyo mipya itahusisha timu 32 na Ligi Kuu England itawakilishwa na Manchester City na Chelsea na itafanyika huko Marekani kati ya Juni na Julai. Fifa bado haijathibitisha viwanja vitakavyotumika kwenye michuano hiyo ambayo fainali yake itakuwa Julai 13.

LONDON, ENGLAND: KEVIN De Bruyne ni mmoja wa mastaa wa maana kabisa ambao wanaweza kuachana na timu zao dirisha la uhamisho wa majira ya kiangazi mwakani katikati ya michuano mipya ya Kombe la Dunia la Klabu.

Michuano hiyo mipya itahusisha timu 32 na Ligi Kuu England itawakilishwa na Manchester City na Chelsea na itafanyika huko Marekani kati ya Juni na Julai. Fifa bado haijathibitisha viwanja vitakavyotumika kwenye michuano hiyo ambayo fainali yake itakuwa Julai 13.

Lakini, mjadala ulioibuka ni kuhusu mikataba ya wachezaji na muda wa michuano hiyo. Michuano hiyo itazidi Juni 30, mwisho wa mwaka wa mikataba mingi ya wanasoka inavyotambuliwa na Fifa.

Wachezaji wengi mikataba yao itafika ukomo Juni 30, hiyo ina maana, wataanza kucheza michuano hiyo wakiwa na mikataba kwenye timu moja, lakini wanaweza kumaliza michuano wakiwa kwenye timu nyingine. De Bruyne anaweza kuwa mmoja wa mastaa hao.

Kinachoelezwa ni wachezaji kibao kutoka kwenye klabu 12 za Uefa zitakazocheza kwenye michuano hiyo wametaka kupata ufahamu kuhusu mikataba yao.

Chanzo kimoja kilifichua: “Kama michuano hiyo ingekuwa majira haya ya kiangazi, Kylian Mbappe angeanza Kombe la Dunia akiichezea PSG na angemaliza mashindano akiwa na Real Madrid.”

Real Madrid ina mastaa watatu kwenye kikosi chao Luka Modric, Dani Carvajal na Lucas Vasquez, ambao wote mikataba yao itafika tamani Juni 30. Bayern Munich yenyewe ina wachezaji sita, Thomas Muller, Manuel Neuer, Joshua Kimmich, Eric Dier, Sven Ulreich na Alphonso Davies ambao wote mikataba yao itakwisha wakati michuano hiyo ya Kombe la Dunia la Klabu ikiendelea.

Davies amekuwa akiwindwa sana na Real Madrid, hivyo anaweza kuanza kwenye michuano hiyo akiwa Bayern na kumaliza akiwa Los Blancos.

Kuna ishu nyingi za kisheria juu ya mikataba haijawekwa sana kuelekea kufanyika kwa michuano hiyo.