Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ngoja tuone… Ni Arsenal au Manchester City

Muktasari:

  • Hata hivyo, mashabiki wa soka wamekuwa na wasiwasi kama mechi hiyo itaendelea kukosa mvuto wa uwanjani kama ilivyotokea mara mbili msimu uliopita. Kwa misimu ya karibuni, Arsenal na Man City zimeonekana timu zinazoshindana kwenye mbio za ubingwa wa Ligi Kuu England.

MANCHESTER, ENGLAND: KIPUTE matata cha Ligi Kuu England baina ya Manchester City na Arsenal kitapigwa leo, Jumapili huko Etihad.

Hata hivyo, mashabiki wa soka wamekuwa na wasiwasi kama mechi hiyo itaendelea kukosa mvuto wa uwanjani kama ilivyotokea mara mbili msimu uliopita. Kwa misimu ya karibuni, Arsenal na Man City zimeonekana timu zinazoshindana kwenye mbio za ubingwa wa Ligi Kuu England.

Lakini, mechi mbili zilizopita baina yao hazikuwa na mvuto kabisa na Kocha wa Arsenal, Mikel Arteta alitumia staili ya Jose Mourinho ya kupaki basi kwenye mechi iliyomalizika kwa sare ya bila kufungana uwanjani Etihad, Machi mwaka huu.

Ilikuwa mara ya kwanza karibu kwa kipindi cha miaka mitatu, Man City kushindwa kufunga bao kwenye mechi ya ligi iliyocheza nyumbani.

Kwenye mechi ya kwanza iliyofanyika Emirates, Oktoba mwaka jana, hali iliyokuwa hivyo hivyo hadi Arsenal ilipopata bao dakika za mwisho la mpira wa kubabatiza la mchezaji Gabriel Martinelli, lililomsaidia Arteta kupata ushindi wake wa kwanza kwenye ligi dhidi ya bosi wake wa zamani, Pep Guardiola. Makocha hao wawili wanaheshimiana sana baada ya kuwahi kufanya kazi pamoja Man City.

Katika mechi 380 za Ligi Kuu England zilizochezwa msimu uliopita, mechi mbili za Man City na Arsenal ndizo zilizokosa msisimko.

Mechi hizo mbili zilikuwa na mashuti matatu tu yaliyolenga goli na hicho ndicho kinachowafanya mashabiki kuwa na wasiwasi wa mchezo wa leo Jumapili, kama mambo yatajirudia na kufanya mchezo uwe mkali kwenye makaratasi na si uwanjani, hasa kipindi hiki Arsenal ikimkosa kiungo wake mwenye ubunifu uwanjani, Martin Odegaard.

Straika wa Man City, Erling Haaland ataingia kwenye mechi hiyo akisaka bao lake la 100 tangu alipojiunga na miamba hiyo ya Etihad, huku akisaka bao la 10 msimu huu baada ya kufunga mara tisa kwenye mechi nne alizochea kwenye ligi.

Tangu ilipopoteza mbele ya Fulham kwenye mkesha wa Mwaka Mpya, Arsenal imecheza mechi 11 ugenini na hiyo sare ya bila kufungana iliyopata Etihad ndiyo mchezo pekee ambao hawakushinda. Je, leo watakapokuwa Etihad, watapaki basi au watafunguka? Ngoja tuone.