Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Van Nistelrooy anampika Zirkzee

Muktasari:

  • Straika huyo Mdachi amerejea Old Trafford kwenda kuongeza nguvu kwenye benchi la ufundi la Man United linaloongozwa na Mdachi mwingine, Erik ten Hag.

MANCHESTER, ENGLAND: RUUD van Nistelrooy ameripotiwa kummegea maujuzi mmoja wa mastaa wapya wa Manchester United siri ya kupandisha kiwango cha soka lake na kuwa moto uwanjani.

Straika huyo Mdachi amerejea Old Trafford kwenda kuongeza nguvu kwenye benchi la ufundi la Man United linaloongozwa na Mdachi mwingine, Erik ten Hag.

Sasa Van Nistelrooy anafanya kazi na mastaa wa kikosi cha kwanza, akiwamo straika mpya aliyenaswa kwa ada ya Pauni 36 milioni dirisha lililopita la usajili, Joshua Zirkzee.

Fowadi huyo, Zirkzee ameweka wazi msaada wa kiufundi anaopata kutoka kwa Van Nistelrooy ni ili kuboresha ubora wake kwenye kufunga mabao.

Hata hivyo, Zirkzee hakutaka kuweka wazi anachofundishwa zaidi na kudai hilo linabakia kuwa siri kwenye uwanja wa mazoezi.

Zirkzee alipoulizwa kitu gani anafanya na Van Nistelrooy, alisema: “Hiyo ni siri. Mambo ni mazuri sana. Alikuwa straika, tunatazama video zake na ilivyokuwa huko nyuma. Kwa namna anavyofanya kazi, ni kitu muhimu sana. Unajifunza mengi kutoka kwake.”

Zirkzee alitua Man United akitokea Bologna, Julai mwaka huu na kusaini mkataba wa miaka mitano. Alifunga bao kwenye mechi yake ya kwanza ya Ligi Kuu England, kwenye ushindi wa 1-0 iliyopata Man United dhidi ya Fulham, lakini baada ya hapo alicheza mechi tano bila ya kufunga. Na usiku wa jana, Jumamosi Man United ilikuwa na kipute kingine cha Ligi Kuu England dhidi ya Crystal Palace huko Selhurst Park. Van Nistelrooy amekuwa akifanya kazi ya kuwanoa mastraika wa miamba hiyo ya Old Trafford. Mdachi huyo aliichezea Man United kwa miaka mitano, akifunga mabao 150 katika mechi 219 kati ya mwaka 2001 na 2005. Alishinda mataji makubwa katika muda huo, ikiwamo Ligi Kuu England kipindi hicho Man United ilipokuwa chini ya Kocha Sir Alex Ferguson.