Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Vigogo Liverpool kumalizana na Diaz

Muktasari:

  • Awali ilielezwa kwamba Diaz mwenye umri wa miaka 27, hana mpango wa kuendelea kusalia Liverpool na badala yake alihitaji kujiunga na Barcelona ambayo ni timu ya ndoto yake

LIVERPOOL imeendelea kufanya mazungumzo na wawakilishi wa winga wao raia wa Colombia, Luis Diaz, 27, baada ya kushindwa kufikia mwafaka katika dirisha lililopita la majira ya kiangazi.

Awali ilielezwa kwamba Diaz mwenye umri wa miaka 27, hana mpango wa kuendelea kusalia Liverpool na badala yake alihitaji kujiunga na Barcelona ambayo ni timu ya ndoto yake

Mkataba wa sasa wa staa huyu unatarajiwa kumalizika mwaka 2027 ni miongoni mwa wachezaji walioonyesha kiwango bora katika kikosicha majogoo hao wa Jiji la Liverpool tangu kuanza kwa msimu huu ambapo amecheza mechi sita za michuano yote na kufunga mabao matano.

Moja ya sababu zilizoripotiwa kwamba zinaweza kumfanya fundi huyu kuondoka katika dirisha lililopita ni baada ya Jurgen Klopp naye kuondoka.


Takehiro Tomiyasu

BEKI wa Arsenal na  Japan, Takehiro Tomiyasu, 25, ameingia kwenye rada za timu nyingine za Italia ikiwemo Napoli ikiwa ni siku kadhaa tangu iripotiwe kwamba anawindwa na Inter Milan.

Arsenal ipo tayari kumwachia staa huyu ambaye hapati nafasi ya kutosha katika kikosi chao cha kwanza lakini kwa kiasi cha pesa kisichopungua Pauni 25 milioni.


Martin Zubimendi 

INAELEZWA Liverpool haina tena mpango wa kurudi mezani kuzungumza na Real Sociedad kwa ajili ya kumsajili kiungo wao raia wa Hispania, Martin Zubimendi  katika dirisha lijalo la majira ya kiangazi.

Liverpool ilionekana kuwa na uhitaji sana na kiungo huyu mwenye umri wa miaka 25, katika dirisha lililopita lakini ilishindikana kwa kile kilichodaiwa kwamba ni masuala ya maslahi.


Joan Garcia

ARSENAL huenda ikarudi tena mezani kuzungumza na Espanyol katika dirisha lijalo la majira ya baridi ili kuipata huduma ya kipa wa timu hiyo na Hispania, Joan Garcia ambaye mwenyewe amethibitisha kwamba ni kweli washika mitutu hao walitamani kumsajili.

Garcia mwenye umri wa miaka 23, anatakiwa na Arsenal kwa ajili ya kuziba pengo la Aaron Ramsdale ambaye ametimkia Southampton.


Rayan Cherki

LICHA ya kuhusishwa na timu mbalimbali ikiwemo Liverpool, Tottenham na Paris St-Germain kiungo wa Olympique  Lyon, Rayan Cherki anatarajiwa kusaini mkataba mpya wa kuendelea kuitumikia Lyon hadi mwaka 2027.

Inaelezwa mabosi wa Lyon hawana mpango wa kumuuza staa huyu ambaye mkataba wake wa sasa unamalizika mwisho wa msimu huu.


Baris Alper Yilmaz

NOTTINGHAM Forest inawafuatilia kwa karibu  mastaa wawili kutoika Uturuki ambao ni winga wa Galatasaray, Baris Alper Yilmaz, 24, na straika wa Besiktas, Semih Kilicsoy, 19, ambao inaweza kuwasajili katika dirisha lijalo la majira ya kiangazi.

Mkataba wa  Baris unatarajiwa kumalizika mwaka 2027, wakati ule wa Semih ukimalizika mwaka 2028.


Josh Acheampong

NEWCASTLE United  inatarajia kutuma ofa kwenda Chelsea kwa ajili ya kumsajili  beki wa timu hiyo Josh Acheampong  katika dirisha lijalo la majira ya baridi.

Josh ambaye anaichezea timu ya taifa ya vijana ya England huenda akajiunga na wababe hao kwa mkopo wa nusu msimu.


Joel Matip

BOURNEMOUTH , Fulham na Wolves zimeendelea kupambana kwa ajili ya kuiwania saini ya beki wa zamani wa Liverpool na Cameroon, Joel Matip, 33, ambaye kwa sasa yupo huru baada ya kuachana na Liverpool mwisho wa msimu uliopita.

Matip ambaye msimu uliopita alicheza mechi 14 za michuano yote, alikuwa akiwindwa na timuj nyingi barani Ulaya.